This is default featured slide 1 title

Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.

This is default featured slide 2 title

Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.

This is default featured slide 3 title

Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.

This is default featured slide 4 title

Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.

This is default featured slide 5 title

Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.

Friday, December 18, 2009

HII NDIYO IKULU YA MAREKANI WAKATI HUU WA SIKU KUU ZA X-MASS NA MWAKA MPYA











BAADHI YA MATUKIO MAKUBWA YALIYOACHA GUMZO DUNIANI MWAKA 2009


Rais wa Marekani Barack Hussein Obama akila kiapo cha kuwa raia wa 44 wa taifa hilo, akishuhudiwa na mkewe Michelle Obama ambaye alimshikia mumewe Biblia, huku mabinti zake wawili, Malia Obama na Sasha Obama wakishuhudia, tukio hili lilifanyika katika eneo la West Front of the Capitol katika Ikulu ya Washington, DC mnamo Januari 20, mwaka huu 2009. (Picha na Chuck Kennedy-Pool wa IFP).


Vertie Hodge, (74) akilia siku kuapishwa kwa rais Obama, hili lilikuwa ni moja ya matukio makubwa ambayo dunia iliweza kulishuhudia. Katika maelezo yake mwanamama huyo alisema kuwa hilo lilikuwa ni tukio kubwa na lakistoroa katika maisha yake kwania amaamini ndoto za wanaharakati za mwanzoni wa kuwakomboa waafrika kama Dk. Martin Luther King, Jr zitakuwa zimetimia licha ya ukweli kwamba hivi sasa wengi wao wameshafariki dunia.Hii ilikuwa ni Januari 20.


Binti wa mezi 16, Aubrey Melton, akiwa sambamba na mama yake akitoa heshima za mwisho kwa baba yake Larissa, ambaye alifariki akiwa kwenye operasheni za kijeshi nchini Afghanistan. Askari huyo ni moja ya wanajeshi mamia wanaokufa kila wakati nchini Afghanistan kutoka mataifa ya Ulaya, Hii ilikuwa ni Juni 27 katika mji wa Illinois nchini Ujerumani.


Mpiga picha wa shirikka la habari la Ufaransa (AP), Emilio Morenatti akichukua picha baada ya kutua katika Chuo kikuu cha Maryland Medical Center akielekea Kernan Orthopaedics and Rehabilitation Hospital iliyopo mjini Baltimore hii ilikuwa baada ya kujeruhiwa katika mlipuko wa bomu nchini Afghanistan. Hii ilikuwa ni Jumanne ya Agosti 25.


Askari wa usalama wa nchni Msumbiji wakijaribu kutuliza mashabiki wa soka waliokuwa wanashangilia timu ya taifa hilo wakati ikipambana na Kenya katika michezo wa kuwania kufuzu Kombe la dunia mwakani nchini Afrika Kusini, mechi hiyo ilifanyika jijini Maputo, Septemba 6 mwaka 2009.



Askari jeshi wa China ajimrudisha dirishani binti alioyetaka kumrusha mwanae gorofani ili afe, hata hivyo jaribio hilo lilikwama kutokana na polisi kutata taarifa hizo mapema kabla ya tukio hilo kutokea. Hii ilikuwa ni Julai 7 katika jimbo la Chengdu, Sichuan


Msichana akiwa nje ya nyumba hao ambayo ileharibika kutokana kuwepo kwa kimbungha aina ya Aila katika eneo la Satkhira Kusini Magharibi mwa Bangladesh, Juni 2.


Maafisa wa Polisi wa Iran akipambana na waandamanaji wanaliokuwa wanapinga matokeo ya uchanguzi mkuu wa rais nchi hiyo tukio hilo lilifanyika mjini Tehran, Juni 13.

Saturday, November 28, 2009

NONDOZZZZZZZ



Ilikuwa siku ya furaha kwa Mdau SARAH ERASTO LUSHU (KULIA) baada ya kutunukiwa Stashahada ya Juu ya Uhasibu kutoka Chuo cha Usimamizi wa fedha (IFM) jijini Dar wa Salaam, Ijumaa iliyopita.

Pembeni yake ni mhitimu mwenzake, JANE ZACHWA ambaye yeye katunukiwa Stashada ya juu ya Kodi, kutoka Chuo hicho hicho.Gazeti ndatu hili (Blog) ya wanajamii inawapa hongera kwa maana huo ndiyo ukubwa, ila ongozeni juhudi katika kupata nondo nyingine zaidi.

Monday, November 23, 2009

LIBENEKE LA FISI AFRIKA YA KATI

AMA KWELI UKISTAAJABU YA MUSA UTAYAONA YA FIRAUNI. Wahenga naamini kwamba hawakukusea kusema msemo huu kwa maama katika nchi ya Jamhuri ya Afrika ya Kati, kumeibuka kundi la vijana wanaofuga Fisi na Nyani kwa kama sehemu ya kujipatia kipato kwa watu na wageni kutoka mataifa mengine ambao wanashangaa aina hiyo mpya ya maisha, hasa kwa hapa Afrika.









Saturday, November 21, 2009

Sarah Mvungi sasa ni Desemba 13



Muimbaji wa nyimbo za Injili nchini Sarah Mvungi hivi sasa yupo kwenye mikakati ya mwishomwisho ya kutoka na albam yake ya kwanza iitwayo Yesu Asante.

Akizungumza na safu hii, Mvungi alieleza kuwa kila kitu kipo sawa na uzinduzi huo utafanyika kwenye Kanisa la Christin Fellowship Sinza jijini Dar es Salaam.

RAYMOND JACKSON ALONGA BIASHARA YA MUZIKI WA INJILI



Muimbaji wa nyimbo za Injili Tanzania Raymond Jackson (PICHANI JUU) amewataka waimbaji wenzake wa nyimbo za Injili kuachana na kuufanya muziki huo kuwa wa biashara ila wafanye kwa ajili ya kulitangaza jina la Yesu Kristo.

Saturday, November 14, 2009

ULAJI WA NYOKA AFRIKA MAGHARIBI

KATIKA Mataifa mengi duniani na hasa ya Afrika, Nyoka ameekuwa ni mnyama hatari kwa maisha ya binadamu, lakini kwa jamii moja kwenye ukanda wa Afrika Magharibi hali imekuwa ni tofauti kwa maana wamekuwa wakitegemea ulaji wa nyoka saka wakatio wa kiangazi ambapo wannyama wengine wanakuwa wamepungua.

Zifuatazo ni picha za wanajamii hao wakiwa katika mawindo ya ufatutaji wa mnyama huyo hatari. Hapa wanaonekana wakiwa na Amaconda moja ya nyoka wakubwa na hatari zaidi duniani.
.













Friday, October 9, 2009

Ambele Chapanyoka atua mbeya

Zifuatazo ni picha mbalimbali za Ambele Chapanyota kabla ya kuoka na baada ya kuokoka.






Muimbaji mahiri wa nyimbo za Injili, Ambele Chapanyota anatarajiwa kuzindua albam yake iitwayo Ni Yesu tu, kazi ambayo inatafaika katika Uwanja wa Sokoine mkoani Mbeya mapema mwenzi Novemba.

Akizungumza na mtandao huu, Chapanyota alisema kuwa katika wakati huu anatarajia kufanya mambo ya tofauti na ilivyokuwa katika zinduzi zilizopita ikiwemo ile ya jijini Dar es Salaam mwaka jana.

"Natarajia kutoka tofauti safari hii, hii ni kwa sababu nakuja kufanya uzinduzi wangu katika mkoa wa Mbeya ambao ndiyo niliyozaliwa na niaoishi, hivyo wakazi wa hapa walioniomba kufanya hsuala hili" alisema Chapanyota.

Thursday, July 23, 2009

Ni zamu ya Joshua John Mlelwa kung'ara






(Joshua John Mlelwa akiwa kwenye jukwaa pamoja na Kundi la Kijitonyama Upendo Group katika moja ya matamasha ya Injili yaliyofanya nchini Tanzania.

Na Mdau wetu

MAKUNDI mengi ya muziki wa Injili nchini Tanzania yamekuwa ni nguzo muhimu katika kulea vipaji vya waimbaji wengi wa muziki huu. Joshua John Mlelwa ni miongoni mwa vipaji vingi hapa nchini vilivyokulia kwenye mikono ya kundi.
Kabla ya kutoka kama muimbaji binafsi, Joshua amekuwa kwenye Kundi la Kijitonyama Upendo Group (KUG) tangu mwaka 1999.
Kabla ya kuwemo kwenye kundi hilo Joshua alikuwa akiimba kwenye Kwaya ya Vijana ya Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) Usharika wa Sumbawanga mwaka 1992 na wakati huo alikuwa akisoma shule ya sekondari ya Mazwi iliyopo mkoani Rukwa.
Baadhi ya kazi alizofanya pamoja na KUG ni pamoja na Mungu Anakupenda ambayo ilikuwa ni albamu yenye nyimbo tisa ndani yake ambazo ni Haleluya, Njooni Kwangu, Tutapataje Kupona na nyingine nyingi.
Pia waliweza kutoa albamu iitwayo Maombolezo iliyokuwa na nyimbo nane, na hii waliitoa wakati wa kifo cha Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere, iliyokuwa na nyimbo kama Taifa Lako Lakulilia, Tutakukumbuka sana pamoja na Mbona Mapema.
Licha ya kupata mafanikio hayo akiwa ndani ya Kijitonyama Upendo Group, ametoka na albamu mbili. Albamu ya kwanza ameitoa mwaka 2007, iitwayo Yesu Yupo yenye vyimbo nane ambayo ameitoa maalum kwa ajili ya kituo cha kulelea watoto Yatima cha Hananasifu Wilayani Kinondoni jijini Dar es Salaam.
“Unajua ukitaka kufanikiwa ni lazima uhakikishe kuwa unakuwa mtoaji ndiyo maana mimi na mke wangu tuliamua kuwa watoaji kwa kutoa albamu hii kwa gharama zetu na mauzo yote kukiachia kituo hicho bila kuchukua hata shilingi moja,” ameongeza muimbaji huyo.
Baada ya kutoka na albamu ya kwanza Joshua Mlelwa ametoka na kazi mpya iitwayo Shaloom yenye nyimbo nane ambazo ni Shaloom, Apewe Sifa Bwana, Niko Juu, Heri Niwe na Wewe pamoja na nyingine nyingi.
“Baada ya albamu ya kwanza hivi sasa nimeshatoa albamu ya pili iitwayo Shaloom na kazi hii nimeifanya ndani ya studio za Shekinah za jijini Dar es Salaam na itakuwa mtaani juma hili,” amefafanua muimbaji huyu mkongwe kwenye muziki wa Injili.
Juu ya mwelekeo wa Muziki wa Injili hapa nchini Joshua ametanabaisha kuwa mwelekeo si mbaya ila wapo baadhi ya waimbaji wa muziki huo wanaoufanya bila kuwa na hofu ya Mungu.
“Watu wanaimba bila kuwa na hofu ya Mungu, wanafanya hivi kwa kuwa wana kipaji lakini hii si sababu ya kuwa mwimbaji wa Injili kwani muziki huu unafanywa kwa ajiliya Mungu. Kwa mfano, hata Michael Jackson amekuwa maafuru ulimwenguni kutokana na kipaji chake cha kuimba lakini hakuwa na hofu ya Mungu, ” amefafanua Joshua ambaye ni baba wa mtoto mmoja.
Kuhsu suala la wizi kwenye sanaa ya Tanzania kwa ujumla, Joshua amesema kuwa ili kulikomesha tatizo hili ni kwa wapenzi wa sanaa kuachana na tabia ya kununua bidhaa bandia na wasanii kuwa na umoja na kushirikiana.
“Wizi bado ni tatizo, kwa mfano nchi nyingi za Afrika Mshariki na Kusini wanatufahamu vema kutokana na kazi zetu ambazo mapato yake hatuyaoni kwa sababu ni kazi za kunakili kutoka kwenye ‘original’,” amesema Joshua.
Baadhi ya nchi ambazo kazi za Kijitonyama Upendo Group zinauzwa kinyemela bila kuwanufaisha ni Malawi, Zambia, Kenya, Botswana, Kenya, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, Burundi na Rwanda.

GAMA WAUSHUKIA MUZIKI WA INJILI




MNENDO wa muziki wa Injili kukubalika kwa mashabiki na wapenzi wake kwa sasa unachangiwa na mambo mbalimbali ambayo ni uimbaji, utunzi na utayarishaji ulio bora.
Gamaliel Daniel Mwasumbi ni miongoni mwa waimbaji ambao wamewezesha suala la uimbaji Tanzania kubadilika na kuwa wa aina yake kwa kuwa wakati anaanza kazi hii yeye na wenzake, Godwin Gondwe na David Robert waimbaji binafsi walikuwa wachche hivyo kujikuta wakiwa na mzigo wa kuhakikisha injili inawafikia watu wengi zaidi.
Katika mazungumzo yake na mdau wa tanzaniacelebrity.com Gamaliel ambaye wengine wanamtambua kama Gama anasema kuwa kwenye huduma hii ya uimbaji baadhi ya mambo hayaendi sawa hivyo kuna haja ya kuwa na neon la uponyaji kwa ajili ya waimbaji na watayarishaji wa muziki wa Injili.
Mambo ambayo Gama anayaona kama ni kikwazo kwenye muziki wa Injili ni pamoja na baadhi ya waimbaji kufanya huduma ya Injili kwa kulenga pesa badala ya kumtumikia Mungu kama ilivyokuwa hapo awali.
“Misingi ya awali kwenye uimbaji wa nyimbo za Injili umevunjwa, kwa maana zamani uinjilisti kwa njia ya uimbaji ilikuwa ni kazi ya wito lakini kwa sasa nashangaa eti muimbaji anaitwa mahali anaanza kuweka masharti mbalimbali ikiwemo suala la kutaka kulipwa,” amesema muimbaji huyo.
Kadhalika Gama ameelezea juu ya utunzi bora wa mashairi kwa kusema kwamba muziki wa Injili si mipasho hivyo waimbaji wanatakiwa kutunga nyimbo zitakazookoa roho za watu kwani hiyo ndiyo kazi ya muziki huo katika jamii.
Amefafanua kuwa kamwe Mungu hana hasara kwa maana amejitosheleza na hivyo kama watu watashindwa kuimba katika roho na kweli ataendelea kuwa Mungu.
“Waimbaji tuzingatie huduma kwa kutunga nyimbo zitakazoweza kuokoa roho za watu kwani bila kufanya hivyo mwisho wa siku tutadaiwa, lakini ninachopenda kuongezea ni kwamba kamwe Mungu hana hasara kama tukiacha kumuimbia, vile vile tusiimbe mipasho,” ameongeza Gama.
Wakati huo huo Gama ameeleza kuwa watengenazaji wa muziki huo kwenye studio (producers) wamekuwa hawaangalii ubora bali fedha imekuwa ni kichocheo kikubwa katika kufanya kazi, jambo linalochangia kutoa kazi zilizo chini ya kiwango.
Licha ya hali hiyo Gama ameongeza kuwa baadhi ya watangazaji kwenye vituo vya redio na televisheni za Kikristo wamekuwa wakiendekeza vitendo vya rushwa kwa waimbaji jambo linalosababisha wale wasiokuwa na uwezo wa kifedha kazi zao kushindwa kusikika kikamilifu.
Gama ambaye kwa sasa anakuja na albamu ya peke yake baada ya kufanya kazi na waimbaji wenzake kwenye Kundi la Yahweh Music linaloundwa na David Robert, Godwin Gondwe pamoja na yeye Gama, amesema kuwa kazi yake hii itakuwa ni tofauti kutokana na kujaza vionjo vya sehemu mbalimbali duniani.
“Albamu yangu mpya itakuwa na mchanganyiko wa vionjo vya Kihindi na Kisenegal na imepewa jina la Usinipite na ina jumla ya nyimbo 12 ambazo ni Mwenye Enzi, Mungu Mkuu, Tunakutukuza, Usinipite, Usisahau, Amen na nyingine,” ameeleza Gama.
Kabla ya kutoka kivyake Gama aliyekuwa kwenye Kundi la Yahweh Music yeye na wenzake walitoa na albamu iitwayo Baba iliyotoka mwaka 2003 na ilikuwa imebeba jumla ya nyimbo 10 ambazo baadhi yake ni Baba, Haleluya Hosana, Nakupenda, Bwana Atafanya Njia na nyinginezo nyingi.
Baadaye alienda jijini Nairobi nchini Kenya akifanya shughuli za muziki wa Injili pamoja na masomo na hivi sasa amerejea nyumbani akiwa na mke aitwaye Rose Boke pamoja na mtoto mmoja wa kiume aitwaye Ntimi.
“Napenda kuwashukuru wadau mbalimbali waliowezesha mimi kufika hapa na wanaendelea kukuza muziki wa Injili hapa nchini, nao ni Eric Shigongo Mkurugenzi wa Global Publishers, vyombo vya habari pamoja na wadau wengine,” amesema Gama.

Wednesday, July 22, 2009

mdau Seppy


Mdau Seppy (kushoto) akiwa na mdau mwenzake wakiendeleza libeneke la mikono's. Seppy ni mmoja wa wadau waliopiga nondo pale VOSA SEKONDARI MIAKA ILEE AMBAPO KWA SASA INAJULIKANA KAMA DAR ES SALAAM CHRISTIN SEMINARY, wakati huo kulikuwa na wadau kama Peris Majura, Kakore, Evelin Komu, Grace Sewe Decha kwa sasa ni waifu wa mtu, Hilda Silas naye ameuaga ukapera juzi juzi tu, du! kweli tumetoka mbali naomba tuwasiliane...!.