This is default featured slide 1 title

Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.

This is default featured slide 2 title

Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.

This is default featured slide 3 title

Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.

This is default featured slide 4 title

Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.

This is default featured slide 5 title

Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.

Tuesday, July 31, 2012

mashabiki kupiga kura kura hapa

Mashabiki wa soka kuanzia leo wanaweza kupiga kura kumchagua mchezaji bora wa mwaka 2012.

Utaribu wa kupiga kura ni kwamba, unatakiwa kuingia kwenye mtandao huu au blong nyingine ikiwemo fullshangwe, issamichuzi, jiachie,sportslady, kingkif, janejohn5,bongostarz pamoja, twitter na face book.


Man Utd yachafuka fedha


LONDON, England

KLABU ya Manchester United, imeingia mkataba wa miaka saba na Kampuni ya kutengeneza magari ya nchini Marekani ya General Motors ambao utaanza kufanya kazi rasmi katika msimu wa mwaka 2014/15.

Mkurugenzi wa biashara wa klabu ya Manchester United, Richard Arnold, alisema kuwa ni moja ya mafanikio kupata mkataba wa muda mrefu ambao utakuwa na manufaa makubwa kwa klabu.

“Hili ni jambo jema kupata mkataba wa muda mrefu kiasi hiki. Tulikutana na Chevrolet kwa muda wa wiki sita tu, lakini waliweza kufanya jambo kubwa kiasi hiki ambalo lina faida kwa pande zote ambao utasaidia kuwafikia mashabiki wetu zaidi ya milioni 659 kote duniani.

Kwa upande wake, Alan Batey,  kutoka kampuni ya General Motors kwa upande wa Marekani ya Kaskazini,  alisema kwamba wamefurahi kuunganisha watu duniani kwa kutumia Manchester ambapo bidhaa yetu ya Chevrolet itafikia watu wengi zaidi.

“Kwa mwendo huu naamini tunaweza kuwafikia mashabiki wengi zaidi, lakini pili bidhaa yetu inaweza kuwafikia watu wengi zaidi duniani, tofauti na awali ambapo tusingeweza kufika kutokana na sababu mbalimbali.

“Tunajua kwamba chini ya uongozi wa Alex Ferguson tunaimani kubwa kwamba bidhaa yetu itawafikia watu wengi kwa ukaribu zaidi,” alikaririwa bosi huyo.

Mkataba huo ni wa kitita cha pauni milioni 210 ambazo ni zaidi ya Sh bilioni 525, ambao utafunika wa sasa na Kampuni ya AON.

Kutokana na tangazo hilo, imefanya kuongezeka kwa nguvu ya hisa kwenye soko la kimataifa la hisa la Marekani jambo litakalowezesha kuvutia wanahisa wengi.

Aidha kiasi cha pauni milioni 30 ndicho kitakachokuwa kinatolewa kwa mwaka kwa ajili ya kuchapisha jezi za klabu hiyo kila msimu, ambapo sasa imevuka ule wa mabingwa wa zamani wa Ulaya Barcelona Qatar Foundation, ambapo inatumia kiasi cha pauni milioni 25 kwa mwaka kwa ajili ya machapisho ya jezi kila mwaka.

Mkataba wa sasa wa Manchester United  na AON (jezi mpya pichani) unafikia kiasi cha pauni  milioni 20 kwa mwaka huku ule wa awali na AIG  ulikuwa wa pauni milioni 14 kwa mwaka hali inayoonekana kukua kwa mtaji kila mkataba na kampuni mpya.

Kutokana na  mkataba huo huenda inaongeza nguvu kwenye mikakati yake ya usajili ambayo imelenga kuwasajili, Robin van Persie  kutoka Arsenal  kwa dau la pauni milioni 15 huku Mbrazil Lucas Moura (19) kutoka klabu ya Sao Paulo ya Brazil kwa gharama ya pauni milioni 30. 
Man United na jezi mpya.

Sunday, July 29, 2012

wazalendo best footballer of the year

Wednesday, July 18, 2012

BREAKING NEEEEEWZ!!! BOT YA SEA GAL INAZAMA KLM CHACHE KUTOKA UNGUJA


Habari zilizoufikia mtandao huu wa www.sufianimafoto.blogspot.com, zinasema kuwa Boti ya Sea Gal, inazama katika moja kisiwa kilicho karibu na kilometa chache kutoka Kisiwa cha Unguja, hivi sasa tayari Boti  tatu za Kilimanjaro zimefika eneo la tukio kwa ajili ya kutoa msaada wa kuokoa watu mahala hapo. Lakini habari zisizothibitihswa mpaka sasa zinasema kuwa wengine kati ya waliopo eneo hilo wanasema kuwa boti hiyo inawaka moto na wengine wakisema kuwa inazama.

Leo ni siku ya kuzaliwa Mzee Nelson Mandela

Rais wa zamani wa Marekani, Bill Clinton akimtembelea Rais wa zamani wa Afrika Kusini, Nelson Mandela nyumbani kwake Qunu, katika picha hii iliyopigwa jana (Julai 17, 2012). Mandela anasherehekea kutimiza umri wa miaka 94 leo Julai 18. Picha: REUTERS

MinistrIKULU:Rais Jakaya Kikwete Akutana na Mkuu wa madhehebu ya Shia Ismailia Duniani,H.H. Karim Aga Khan

 Rais Jakaya Mrisho Kikwete akimsindikiza  Mkuu wa madhehebu ya Shia Ismailia duniani,H.H. Karim Aga Khan, wakati alipomkaribisha Ikulu jijini Dar es salaam leo kwa mazungumzo na baadaye chakula cha mchana.
 Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwa katika mazungumzo na  Mkuu wa madhehebu ya Shia Ismailia duniani,H.H. Karim Aga Khan, wakati alipomkaribisha Ikulu jijini Dar es salaam leo kwa mazungumzo na baadaye chakula cha mchana.
 Rais Jakaya Mrisho Kikwete akipeana mikono na  Mkuu wa madhehebu ya Shia Ismailia duniani,H.H. Karim Aga Khan, wakati alipomkaribisha Ikulu jijini Dar es salaam leo Julai 18, 2012 kwa mazungumzo na baadaye chakula cha mchana.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akimlaki na Mkuu wa madhehebu ya Shia Ismailia duniani,H.H. Karim Aga Khan, wakati alipomkaribisha Ikulu jijini Dar es salaam leo kwa mazungumzo na baadaye chakula cha mchana.Picha na IKULU.

Thursday, July 5, 2012

MELI ZA IRANI KUFUTWA NCHINI?


Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe (kushoto) akifafanua jambo katika mkutano na waandishi wa habari, Dar es Salaam leo, kuhusu sakata la baadhi ya meli za Irani zinazodaiwa kupeperusha Bendera ya Taifa ya Tanzania katika Bahari ya Hindi. Kulia ni Katibu Mkuu wa wizara hiyo, John Haule. (PICHA KWA HISANI YA RICHARD MWAIKENDA)

RAIS KIKWETE AONGOZA BAARZA LA MAWAZIRI DODOMA LEO

Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiongea jambo na baadhi ya mawaziri na viongozi waandamizi serikalini  baada ya kuongoza kikao cha Baraza la Mawaziri leo July 5, 2012 katika ukumbi wa TAMISEMI Dodoma.

 



Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiongoza kikao cha  Baraza la Mawaziri leo July 5, 2012 katika ukumbi wa TAMISEMI Dodoma.
PICHA KWA HISANI YA OFISI YA WAZIRI MKUU

WAKAZI 8000 WAFAIDIKA NA HUDUMA ZA BENKI YA DUNIA, MKOA WA RUKWA


Diwani kata ya MWIMBI wilaya MPYA ya KALAMBO Mkoa wa Rukwa Leonard Shalamwana (wa tatu kulia)akimuonesha Mkuu wa wilaya Moshi Mussa Chang'a(wa tatu kushoto) chanzo cha Mradi wa maji utakaogharimu zaidi ya shilingi milioni 158.3 na kunufaisha takribani wakazi 8,000. Mradi huo unadhaminiwa na benki ya dunia, wananchi pamoja na mfuko wa maendeleo wa jimbo la Kalambo. Wengine kutoka kushoto ni Mratibu wa Miradi ya TASAF wilaya John Kiondo na Kaimu Mkurugenzi wilaya Sumbawanga Crispin Luanda. 
NA RAMADHANI JUMA,
AFISA HABARI, SUMBAWANGA
WAKAZI wapatao 8,000 wa vijiji viwili vya Majengo na Mwimbi katika Kata ya Mwimbi wilaya mpya ya Kalambo Mkoa wa Rukwa wanatarajia kunufaika na mradi wa maji safi unatekelezwa katika kata hiyo kwa gharama ya zaidi ya shilingi milioni 158.3.
Mradi huo unadhaminiwa na Benki ya Dunia iliyotoa zaidi ya shilingi milioni 154.4, wakazi wa kata hiyo wamechangia shilingi 2,709,000 na mfuko wa jimbo la Kalambo umetoa shilingi 1,200,000 ili kufanikisha mradi huo.
Akielezea mradi huo mbele ya Mkuu wa wilaya ya Kalambo Moshi Mussa Chang’a, diwani wa Kata ya Mwimbi Leonard Shalamwana alisema kwa sasa mradi huo uko katika hatua ya nne ambayo ni usambazaji wa maji katika vituo vikuu.
Afisa Mtendaji wa Kata hiyo Mosses Nkinda alisema mradi huo utaongeza upatikanaji wa maji kwa wakazi hao na kuongeza kasi ya maendeleo na kukuza hali ya kiuchumi mara utakapokamilika.
Kwa upande wake, Mkuu wa wilaya hiyo Moshi Mussa Chang’a alipongeza utekelezaji wa mradi huo na kuwataka viongozi wa kata hiyo kuhakikisha kuwa unakamilika haraka ili wakazi hao waanze kunufaika nao kama ilivyokusudiwa.

WAZIRI MKUU MIZENGO PINDA NA BUNGENI LEO



Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akisikiliza swali kutoka kwa kiongozi wa Upinzani Bungeni, Freeman Mbowe katika kipindi cha maswali kwa Waziri Mkuu, Mjini Dodoma  Julai 6,2012.(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akiteta na Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongokwenye viwanja vya Bunge Mjini Dodoma Julai 6, 2012.(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akiteta na Mbunge wa Ludewa, Deo Filikunjombe kwenye viwanja vya Bunge Mjini Dodoma Julai 6, 2012.(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

AJISHINDIA JENERETA YA VUMBUA HAZINA CHINI YA KIZIBO


Bw Salvatory Herald wa pili kutoka kushoto alipongezwa na ndugu jamaa na marafiki pamoja baadhi ya wakazi wa tanga waliohudhuria katika hafla fupi ya kukabidhiwa zawadi ya jenereta mpya aliojishindia kupitia promosheni ya VUMBUA HAZINA CHINI YA KIZIBO NA SBL, inayoendeshwa na kampuni ya bia ya Serengeti hapa nchini.

Picha 03 ni bw Salvatory akieleza hisia zake baada ya kukabidhiwa jenereta kutoka sbl.


Meneja masoko wa kampuni ya bia ya Serengeti bw Eben Sauli kushoto ampongeza salvatory Herald baada ya kumkabidhi zawadi ya jenereta aliojishindia .

Okwi mali halali ya Simba, akana kwenda Yanga


Kaburu akiwaonyesha Waandishi mkataba wa Okwi na Simba 


Mkataba wa Okwi na Simba

Vipengele hapo

Kaburu akizungumza na Waandishi wa Habari

Kaburu akiwasikiliza sauti ya Okwi waandishi

Hapa anafafanua jambo

Monday, July 2, 2012

Uzalendo wawakimbiza Wataalamu Zanzibar

Habari zote na Juma Mohammed, MAELEZO Zanzibar
Kukosekana kwa uzalendo na tama ya kipato kikubwa kumetajwa kuwa sababu ya ya baadhi ya wananchi wataalam kuacha kazi Serikali ya Mapinduzi Zanzibar na kukimbilia ughaibuni.
Akijibu swali katika Baraza la Wawakilishi, Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Haji Omar Kheri alikiri kuwepo kwa tatizo la wataalam wa kizalendo kuondoka nchini kwa kutafuta maslahi zaidi nje ya nchi.
 Katika swali la msingi,.  Mwakilishi wa Jimbo la Wawi (CUF) Saleh Nassor Juma alitaka kujua sababu za wataalamu kuendelea kukimbia nchini.
Mwakilishi huyo apamoja na Mwakilishi wa Salum Abdallah Hamad (CUF) wa Matambwe, Rashid Seif Suleiman (CUF) wa Ziwani na Jaku Hashim Ayoub wa Jimbo la Muyuni (CCM) wote walilalamika kuwa serikali inachangia kuwatorosha wataalamu kwa kuwawekea mazingira mabaya ya utendaji kazi na malipo duni.
“Naomba nikubaliane na wajumbe wa baraza la wawakilishi kuwa nchi nyingi zilizopo kwa janga la sahara hukimbiwa sana na wataalamu wake hususan madaktari wakiwemo pia maprofesa na wahadhiri licha ya kulipwa stahiki mbali mbali” alisema waziri Kheri.
Waziri alisema Zanzibar pia imekuwa ikikabiliwa na tatizo la kukimbiwa na wataalamu wake hasa kada ya udaktari hospitali ambao wanakwenda nchi nyengine kupata maslahi mazuri zaidi.
Hata hivyo waziri huyo alisema miongoni mwa sababu zinazosababisha wataalamu kukimbia ni ukosefu wa maslahi bora na vitendea kazi lakini kubwa zaidi ni kukosa uzalendo.
“Serikali imekuwa ikifanya juhudi za kuimarisha maslahi ya watumishi wake na kuanzia mwaka jana wataalamu mbali mbali walirekebishiwa mishahara pamoja na posho wakiwemo madaktari lakini licha ya hilo kutokana na kukosekana uzalendo baadhi ya madaktari wanaondoka” alilalamika waziri huyo.
Waziri Kheri aliwataka wajumbe wa baraza la wawakilishi kusaidia katika juhudi za kuwashawishi wataalamu waliokuwepo nchini kupenda nchi yao na kuwatumikia wananchi huku serikali ikifanya juhudi za kuimarisha maslahi na mazingira bora ya kazi.

MANJI AZUA 'BALAA' TFF, UCHAGUZI YANGA WAINGIA KIZA

Manji anaondoka TFF, umati ukimsindikiza

Sura za huzuni; wanachama wakisikitika nje ya ofisi za TFF

Wanachama wakisikitikia pingamizi la Manji

Ni huzuni tupu

Hakuna anayufurahia 

Kila mtu ana hasira

Yaani watu wamekasirika ile mbaya

Hadi akina mama wana hasira pia

Manji anatoka chumba cha mahojiano

Anaziacha ofisi za TFF

Anapotea

Anawasalimu wazee

Anajadiliana na wazee

Umati unamsindikiza

Anafunguliwa mlango wa gari lake

Anaingia na kupotea

Na Prince Akbar
MAMIA ya wanachama wa klabu ya Yanga ya Dar es Salaam, leo wameandamana hadi makao makuu ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Ilala, Jijini kupinga pingamizi alilowekewa mgombea Uenyekiti wa klabu hiyo katika uchaguzi wa Julai 15, mwaka huu, Yussuf Manji.
Kamati ya Uchaguzi ya TFF, chini ya Mwenyekiti wake, Deo Lyatto leo ilikuwa inapitia pingamizi mbili walizowekewa wagombea, Manji na Stanley Kavela ‘Yono’ anayewania Umakamu Mwenyekiti.
Tangu saa nne asubuhi hadi saa nane mchana, Kamati hiyo ilikuwa inamuhoji Manji ambaye hata alipotoka, ilielezwa alitakiwa kurejea tena.
Manji alitoka mara mbili na kurejea kufuata vielelezo alivyotakiwa kuwasilisha kuhusiana na pingamizi alilowekewa, ambalo vyanzo vinasema ni zito.
Tangu asubuhi wanachama walikuwa ‘kibao’ nje ya Ofisi za TFF, zilizopo ndani ya Uwanja wa Karume, Ilala, Dar es Salaam wakionyesha hasira zao dhidi ya pingamizi hilo, ambalo aliloliweka anafanywa siri.
Wanachama walisikika wakisema kwamba kama Kamati ya Lyatto itamuengua Manji basi hakuna haja ya uchaguzi.
Miongoni mwa waliokuwapo katika wanachama ni wazee wa klabu hiyo, akina Ibrahim Akilimali, Dk Idrisa Katundu na wengineo, wakiwemo wanachama maarufu.
Kuna kila dalili kwamba uamuzi wa kumuengua Manji katika uchaguzi huo litakuwa jambo la hatari kwa klabu hiyo, kwani wanachama tayari wamekwishajenga imani kubwa juu yake.   
Manji mwenyewe alipotoka kwenye chumba cha mahojiano alionekana asiye na furaha hali ambayo ilizidi kuwatia wasiwasi wanachama kwamba huenda kikao hakikuwa kizuri kwake.
 
PICHA NA HABARI KWA ZINATOKA MTANDAO WA BIN ZUBERY