This is default featured slide 1 title

Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.

This is default featured slide 2 title

Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.

This is default featured slide 3 title

Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.

This is default featured slide 4 title

Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.

This is default featured slide 5 title

Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.

Wednesday, February 8, 2012

Jaji Mkuu wa Tanzania Othman Chande Amwapisha Hakimu Mkazi,Katika Mahakama Ya Rufani

Jaji Mkuu wa Tanzania Mhe. Othman Chande akimuapisha Mhe. Musa Francis Esanju kuwa Hakimu Mkazi, katika Mahakama ya Rufani jijini Dar es Salaam, anayeshuhudia (katikati) ni Mhe. Francis Mutungi, Msajili Mahakama ya Rufani Tanzania
Jaji Mkuu wa Tanzania Mhe. Othman Chande(katikati),Jaji Kiongozi,Mhe. Fakih Jundu (Kushoto) na Msajili wa Mahakama ya Rufani, Mhe. Francis Mutungi (kulia)wakiwa katika picha ya pamoja na Waheshimiwa Mahakimu waliokabidhiwa hati ya uteuzi na kuapishwa.Mhe amewaasa kuwa na maadili na kazi yao na kutoa haki sawa kwa wote na kwa wakati.

Taswira Halisi Kutoka Hospitali Ya Taifa Ya Muhimbili Leo Hii Kufwatia Mgomo Wa Madaktari Unaoendelea Hivi Sasa

Ndugu na Jamaa wakiwa kwenye harakati za kumwamisha Mgonjwa wao kutoka hospitali ya Taifa ya muhimbili kufwatia mgomo Mkubwa wa Madaktari
Chumba Cha Wagonjwa kikiwa kitupu
Muonekano wa Wodi Mbalimbali
Chumba cha Wagonjwa kikiwa kitupu
Vitanda vitupu vikiwa Havina wagonjwa kwenye hospitali ya taifa ya muhimbili Kufwatia Mgomo wa Madaktari unaoendelea nchini hivi sasa
Viti vya kubebea Wagonjwa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili vikiwa vitupu kabisa
Koridoro za hospitali ya Taifa ya Muhimbili Zikiwa Tupu Leo hii kufwatia Mgomo wa Madaktari Nchini
Sehemu ya Mapokezi ya Hospitali ya taifa ya muhimbili ikiwa tupu
Bi Annanilea Nkya(Kulia)na kijo Bisimba wa pili Kushoto wakiwa Hospitali ya Taifa ya Muhimbli jijini Dar es Salaam Kujionea hali halisi na athari za Mgomo wa Madakatari unaondelea Nchini.Picha na Habari Legal and Human Rights Centre

Jaji Damian Lubuva:Uchaguzi Mdogo Jimbo La Arumeru Mashariki Kufanyika April Mosi 2012.

Rais Jakaya Kikwete akimpongeza Jaji mstaafu Damian Lubuva nje ya viwanja vya ikulu jijini Dar es Salaam Muda Mfupi baada ya Rais Kikwete Kumwapisha Jaji Lubuva kuwa Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), Ikulu, Dar es Salaam Hivi Karibuni
--
Uchaguzi mdogo wa ubunge katika jimbo la Arumeru Mashariki unatarajiwa kufanyika April Mosi mwaka huu.
Uchaguzi huo utafanyika baada ya jimbo hilo kuwa wazi kutokana na kifo cha aliyekuwa mbunge wake Marehemu Jeremia Solomon Sumari aliyefariki dunia Januari 19 mwaka huu.
Taarifa iliyotolewa na Tume ya Taifa ya uchaguzi leo jijini Dar es salaam imesema pamoja na uchaguzi huo mdogo pia kutakuwepo na chaguzi ndogo za madiwani katika kata za Halmashauri mbalimbali nchini.
Taarifa hiyo ya Tume ya Taifa ya uchaguzi inaonesha kuwa katika uchaguzi mdogo wa ubunge kwenye jimbo la Arumeru Mashariki uteuzi wa wagombea utafanyika Machi 8, na kampeni zitaanza Machi 9 hadi 31 mwaka huu.
Aidha, Tume hiyo pia itafanya chaguzi ndogo za madiwani katika kata nane zilizoko katika halmashauri mbalimbali nchini kufuatia kuwepo wazi kwa nafasi za viti vya madiwani ambazo zimetokana na vifo vya madiwani husika.
Katika chaguzi ndogo za madiwani uteuzi wa wagombea utafanyika Machi 5 na kampeni zitaanza Machi 6 hadi 31 mwaka huu. Kata zitakazohusika kwenye uchaguzi huo ni zile vijibweni-Temeke, Kiwanga-bagamoyo, Kirumba-Mwanza, Logangabilili-Bariadi, Chan’gombe-Dodoma, Kiwira-Rungwe, Lizaboni-Songea na Msambweni-Tanga.
Taarifa hiyo iliyosainiwa na Mwenyekiti wa Tume hiyo Jaji Damian Lubuva imesema kuwa hakutakuwa na kuandikisha wapiga kura kwa ajili ya chaguzi hizo ila daftari la kudumu la wapiga kura lililotumika wakati wa uchaguzi mkuu uliopita litatumika.
Tume inawasisitiza wananchi na vyama vyote vya siasa kuzingatia na kufuata ratiba ya uchaguzi na kujitokeza kwa wingi kushiriki katika mchakato wa uchaguzi kuanzia siku ya uteuzi wa wagombea, kampeni za uchaguzi na siku ya kupiga kura. Vituo vya kupigia kura vitafunguliwa saa 1.00 asubuhi na kufungwa saa 10.00 alasiri

Monday, February 6, 2012

Makamu Wa Rais Dk Gharib Bilal Ikulu Jijini Dar es Salaam Leo

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akipokea zawadi ya kitabu cha China kutoka kwa Balozi wa China nchini Tanzania, Liu Xinsheng, aliyefika ofisini kwake Ikulu Dar es Salaam leo Februari 6, 2012 kwa ajili ya kumuaga baada ya kumaliza muda wake nchini
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akizungumza na Balozi wa China nchini Tanzania, Liu Xinsheng, aliyefika ofisini kwake Ikulu Dar es Salaam leo Februari 6, 2012 kwa ajili ya kumuaga baada ya kumaliza muda wake nchini.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akizungumza na baadhi ya Mabalozi wateule wanaokwenda kufanya kazi nchi za nje walizopangiwa, wakati walipofika ofisini kwake Ikulu Dar es Salaam leo Februari 6, 2012 kwa ajili ya kumuaga kabla ya kwenda kuanza majukumu yao ya kikazi katika nchi walizopangiwa.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiwa katika picha ya pamoja kwa kumbukumbu na baadhi ya Mabalozi wateule baada ya kumaliza mazungumzo nao wakati walipofika ofisini kwake Ikulu jijini Dar es Salaam leo Februari 6, 2012 kwa ajili ya kumuaga kabla ya kuondoa kwenda kuanza majukumu yao ya kikazi katika nchi walizopangiwa. Picha na Muhidin Sufiani-Ofisi ya Makamu wa Rais

Rais Jakaya Kikwete Amjulia Hali Mkuu wa Majeshi Mstaafu Jenerali Ernest Mwita Kyaro


Rais Jakaya Mrisho Kikwete na mkewe mama Salma Kikwete wakimjulia hali Mkuu wa Majeshi Mstaafu Jenerali (mst) Ernest Mwita Kyaro jijini Mwanza asubuhi ya leo Jauary 6, 2012. Jenerali mstaafu Kyaro, ambaye alikuwa mkuu wa majeshi katika serikali ya awamu ya kwanza, amefurahi na kumshukuru sana Rais Kikwete na mkewe kwa kutembelea

Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiongea na wawakilishi wa kundi moja la wachuuzi (machinga) wa jijini Mwanza ambao leo January 6, 2012 walikwenda Ikulundogo ya jiji hilo na kumweleza changamoto zinazowakabiri, ikiwa ni pamoja na ukosefu wa mitaji pamoja na taaluma ya kufanyia biashara. Rais Kikwete ametoa milioni 10 kwa ajili yawamachinga hao kukopeshana mitaji.Picha na IKULU

Kutoka Bungeni Mjini Dodoma


Waziri wa Nishati na Madini William Ngeleja akijibu maswali ya wabunge kuhusu upatikanaji wa umeme wa uhakika nchini na uondoaji wa tatizo la mgawo wa umeme unaoendelea kwenye baadhi ya maeneo nchini na kufafanua kuwa serikali inaendelea na mikakati ya utekelezaji wa miradi mbalimbali ya utoaji wa huduma ya umeme katika maeneo yasiyo na huduma hiyo na kuimarisha uzalishaji wa umeme wa uhakika katika Gridi ya Taifa kupitia vyanzo mbalimbali.

Waziri na Afya na Ustawi wa Jamii Dkt. Hadji Mponda(kushoto) akizungumza jambo na Waziri Mkuu Mizengo Pinda (kulia)ndani ya ukumbi wa Bunge leo mjini Dodoma.

Mbunge wa Kigoma Kusini (NCCR –Mageuzi) David Kafulila akichangia bungen kuhusu namna bora ya ukusanyaji wa mapato kupitia kodi zinazotozwa kwenye makampuni ya simu nchini ili kuongeza mapato ya serikali leo mjini Dodoma.


Naibu spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Job Ndugay akitoa ufafanuzi wa hoja mbalimbali zilizowasilishwa na wabunge wakati wa kikao cha tano cha mkutano wa sita leo mjini Dodoma.
Naibu waziri wa Wizara ya Fedha Gregory Theu (kushoto) akizungumza jambo na Naibu waziri wa Wizara ya Kilimo, Chakula na Ushirika Christopher Chiza (kulia) nje ya ukumbi wa Bunge leo mjini Dodoma.
Waziri wa Fedha Mustapha Mkulo (kulia) akitoa ufafanuzi wa masuala mbalimbali kwa wabunge mara baada ya kumalizika kwa kikao cha tano cha mkutano wa sita leo mjini Dodoma.Kutoka kushoto ni mbunge wa Kigoma Kaskazini Zitto Kabwe na Davidi Kafulila (wa pili kutoka kushoto) kutoka Kigoma kusini. Picha na Aron Msigwa –MAELEZO.

Naibu Waziri Wa Viwanda na Biashara Lazaro Nyalandu,Mwenyekiti wa CHADEMA Freeman Mbowe na Ezekiel Wenje(CHADEMA)Watembelea Ubalozi wa Tanzania Nchini


Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara, Mh. Lazaro Nyalandu akisaini kitabu cha wageni.
Kiongozi kambi ya Upinzani Bungeni, Mh. Freeman Mbowe akisani kitabu cha wageni.
Waziri kivuli wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kiamtaifa, Mh. Ezekia Wenji akitia saini kitabu cha wageni.
Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara wa Tanzania, Mh. Lazaro Nyalandu (kulia) akiwa pamoja na Waziri kivuli Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Ezekia Wenje wakiwa kwenye mkutano na Maofisa wa Ubalozi wa Tanzania Nchini Marekani, Ijumaa February 3, 2012 katika Ofisi za Ubalozi wa Tanzania, Washington, DC.
Kushoto ni Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara, Mh. Lazaro Nyalandu akiwa na Kiongozi wa kambi ya Upinzani Bungeni, Mh. Freeman Mbowe (CHADEMA).
Kushoto na Dr, Switebert Mkama akiwa na Afisa Mindi Kasiga.
Kushoto ni Afisa Edward Masanja akiwa na Afisa Agnes Lusinde.
Kutoka kushoto ni Maafisa, Brigedia jenerali Maganga, Mama Kiju na Suleiman Saleh wakiwa katika mkutano
Kutoka kushoto ni Afisa Mindi Kasiga, Afisa Suleiman Saleh, Dr Switebert Mkama, Kiongozi wa kambi ya Upinzani Bungeni, Mh. Freeman Mbowe, Waziri kivuli wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mh. Ezekia Wenje, Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara, Mh. Lazaro Nyalandu, Afisa Kiju, Kaimu Balozi, Mh. Lily Munanka, Afisa Abbas Missana, Afisa Agnes Lusinde, Afisa Edward Masanja na Brigedia Jenerali Maganga wakiwa katika picha ya pamoja.

MAKAMU WA RAIS DK.GHARIB BILAL MGENI RASMI SHEREHE ZA MKESHA WA MAULID VIWANJA VYA MNAZI MMOJA JIJINI DAR ES SALAAM


Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiteta jambo na Waziri Mkuu Mstaafu Edward Lowasa, wakati wakiwa katika sherehe za mkesha wa Maulid, zilizofanyika usiku wa kuamkia leo, jana usiku Februari 04, 2012, katika viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam.


Muumin wa dini ya kiislam kutoka Msikiti wa Suni Hanafi wa jijini Dar es Salaam, Muzamil Chaki, akiimba Qaswaida jukwaani kutoa burudani wakati wa mkesha wa sherehe za Mauilid zilizofanyika katika Viwanja vya Mnazi Mmoja jijini jana usiku Februari 04, 2012.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akipokea kadi ya mwanachama wa CHADEMA, Mshindo Kisike, aliyekuwa Katibu mkuu na mweka hazina wa chama hicho Kata ya Kibaha, aliyejiengua na kujiunga na CCM, wakati Makamu akimalizia ziara yake ya Mkoa wa Pwani Wilayani Kibaha, jana Februari 04, 2012.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisalimiana na Rais Mstaafu wa awamu ya pili, Ali Hassan Mwinyi, wakati alipowasili kwenye viwanja vya Mnazi Mmoja katika shambrashambra za mkesha wa sherehe za Maulid, jijini Dar es Salaam jana Februari 04, 2012 usiku.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal(katikati) Rais Mstaafu wa awamu ya pili, Ali Hassan Mwinyi na Waziri Mkuu Mstaafu, Edward Lowasa, wakiwa katika sherehe za mkesha wa Maulid, zilizofanyika usiku wa kuamkia leo, jana usiku Februari 04, 2012, katika viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam.Picha na Muhidin Sufiani-Ofisi ya Makamu Wa Rais

Taswira Mbalimbali Za Rais Jakaya Kikwete Katika Sherehe Za Miaka 35 ya CCM Mwanza

Rais Jakaya Kikwete akihutubia maelfu ya wana CCM na wakaazi wa Mwanza leo katika kuadhimisha miaka 35 ya CCM uwanja wa Kirumba
Mwenyekiti wa CCM, Rais Jakaya Kikwete, Mama Salma Kikwete wakiongoza matembezi hayo kutoka kwenye Ofisi ya CCM mkoa wa Mwanza hadi viwanja vya Furahisha jijini Mwanza akiwa na viongozi wa ngazi ya juu wa CCM. Kutoka Ofisi hiyo hadi kwenye viwanja ni umbali wa kilometa tatu.
Rais Kikwete akimsalimia Katibu Mkuu wa CCM mstaafu, Philip Mangula kabla yamatembezi kuanza Ofisi ya CCM mkoa wa Mwanza. Kulia ni Katibu Mkuu Mstaafu Yussuf Makamba.
Rais Kikwete akimsalimia Nape Nnauye Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi Nape Nnauye kabla ya matembezi hayo.
Mama Salma Kikwete na Spika Anne Makinda na wakinamama wakisherehekea miaka 35 ya CCM baada ya kukunwa na wimbo wa Vicky kamata.Rais Jakaya Kikwete akiongoza matembezi ya mshikamano mapema asubuhi
Rais Jakaya Kikwete akisalimia vikundi mbalimbali vya burudani na wana CCM na wakaazi wa Mwanza leo katika kuadhimisha miaka 35 ya CCM uwanja wa Kirumba
wakaazi wa Mwanza leo katika kuadhimisha miaka 35 ya CCM uwanja wa Kirumba
wakaazi wa Mwanza wakiwa kwenye maandamano ya pikipiki katika kuadhimisha miaka 35 ya CCM uwanja wa Kirumba
Wageni mbalimbali walioudhuria sherehe za miaka 35 ya CCM uwanja wa Kirumba Mkoani Mwanza leo.Picha na IKULU