
UTANGULIZIMheshimiwa Spika, kwa maslahi ya umma wa Watanzania, napenda kuchukua nafasi hii kumshukuru Mwenyezi Mungu kwa kuniwezesha kuwepo hapa leo, kuwasilisha Maoni na Mapendekezo ya Kambi rasmi ya Upinzani, kuhusu Wizara ya Mambo ya Ndani, kwa mujibu wa kanuni ya 99(7) ya Kanuni za Kudumu za Bunge, Toleo la mwaka 2007.Mheshimiwa Spika, natoa pia shukurani zangu za dhati kwa familia yangu, Mke wangu Neema Lema, watoto wangu, Allbless Lema na Brilliant...