Mwanamitindo Naomi Campbell, anatarajiwa kutoa ushahidi katika mahakama ya jinai huko the Hague kwenye kesi inayomkabili rais wa zamani wa Liberia Charles Taylor.
Bi Campbell inadaiwa alipokea almasi kutoka kwa rais huyo wa zamani kama zawadi mwaka 1997 -- ingawa amekanusha.
Bwana Taylor anayekabiliwa na kesi ya mauaji ya kivita katika mahakama maalum kuhusu Sierra Leone huko the Hague, inadaiwa alimkabidhi Bi Campbell almasi kama zawadi mnamo mwaka huo akiwa nchini Afrika kusini kwa mwaliko wa rais mstaafu Nelson Mandela.
Hata hivyo Taylor amekanusha madai hayo na ndio sababu kuu ya bi Campbell kutakiwa kutoa ushahidi katika kesi hiyo.
Madai hayo pia yamesemekana kuwa sababu ya kesi dhidi ya Yaylor kwa vitendo vyake, wakati wa vita vya wenyewe kwa wenyewe katika nchi jirani ya Sierra Leone.
Upande wa mashtaka ungetaka kuthibitisha kuwa bwana Taylor alihusika katika biashara ya kubadilishana silaha na kupewa Almasi zilizopatikana kutokana na vita vya wenyewe kwa wenyewe nchini Sierra Leone.
0 comments:
Post a Comment