Saturday, June 11, 2011

Usajili hatari Tanzania Bara



Nyota mahiri wa Tanzania, Mohamed Selemani Mwimbe, aliyekuwa anacheza soka la kulipwa nchini Swaziland ametua nchini hivi karibuni na sasa anawaniwa na klabu mbalimbali za Ligi Kuu Tanzania Bara ikiwemo Yanga, Moro United na Villa Squard zote za jijini Dar es Salaam.

Mwimbe maarufu kama Mswati (21) ni miongoni mwa nyota ambao wamekuwa gumzo katika usajili wa Tanzania msimu huu huku akitarajiwa kutua katika klabu moja kati ya hizo. Klabu aliyokuwa akiitumikia ni akiitumikia ni Bambane Highlanders United.

Akizungumza na Mtandao huu, Mswati alisema kuwa ana imani kwamba wakati wa mafanikio katika soka umeendelea kuwa mzuri kwake huku akieleza kuwa Watanzania wanatakiwa kuwaunga mkono vijana wao.

0 comments: