Naibu Waziri Wa Ujenzi Dk Harrison Mwakyembe akishuka katika madhabahu mara baada ya kumalizika kwa ibada hiyo Jana
Waziri wa Afrika Mashariki Mbunge wa Urambo Samwel Sitta na akishuka katika madhabahu mara baada ya kumalizika kwa ibada jana
Waziri wa Afrika Mashariki na Mbunge wa Urambo Samwel Sitta akiongea katika ibada hiyo na kumkaribisha Dk Harrison Mwakyembe ili kuzungumza machache na waumini wa kanisa hilo na kutoa ushuhuda wake.
Mbunge wa Kahama Bw. James Lembeli kushoto , akizungumza na Dk. Harrison Mwakyembe wakati wa ibada hiyo jana
Dk. Harrison Mwakyembe wa pili kutoka kulia akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya wabunge, kushoto ni Mbunge wa Same Mashariki Mama Anne Kilango Malecela, Waziri wa Afrika Mashariki Samwel Sitta na Mbunge wa Kahama Bw. James Lembeli.Dk Harrison Mwakyembe Mbunge wa Kyela na Naibu Waziri wa Ujenzi katika ibada iliyofanyika jana kwenye kanisa hilo na kuhudhuriwa na Waziri wa Afrika Mashariki mzee Samwel Sitta na baadhi ya wabunge kadhaa, Mzee Samwel Sitta amesema Mwakyembe amekwenda kanisani hapo ili kutoa ushuhuda kuhusu ugonjwa wake kwa ujumla. Dk. Harrison Mwakyembe ametoa ushuhuda akimshukuru mungu kwa kumbariki na kuendelea kumpa nguvu juu ya afya njema, Mwakyembe ambaye alikuwa amevalia kofia na Glovu katika mikono yake, ameongeza kwamba tangu alipokuwa ameondoka kwenda nchini India kwa matibabu Oktoba 9 mwaka jana hakuwahi kuvaa viatu, lakini leo amevaa, hivyo akamshukuru mungu kwa miujiza yake.Picha na John Bukuku
0 comments:
Post a Comment