Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Pensheni kwa
Watumishi wa Umma (PSPF), Adam Mayingu akizungumza na waandishi wa habari
wakati wa ziara ya viongozi wa Manispaa ya Ilala pamoja na wadau wa mfuko huo
walipotembelea mradi wa nyumba za ambazo zitakopeshwa kwa wanachama wake zilizopo Buyuni, Chanika nje kidogo
ya Dar es Salaam jana. (Picha na Dande JR)
Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa
Mfuko wa Pensheni kwa Watumishi wa Umma (PSPF), Adam Mayingu (wa tatu kulia)
wakati wa ziara ya viongozi wa Manispaa ya Ilala pamoja na wadau wa mfuko huo
walipotembelea mradi wa nyumba za PSPF zilizopo Buyuni, Chanika nje kidogo ya
Dar es Salaam
Kaimu
Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Pensheni kwa Watumishi wa Umma (PSPF) Adam
Mayingu (katikati) akiwaonesha maofisa wa Jeshi la Polisi moja ya nyumba
491 zilizopo katika mradi wa ujenzi wa nyumba za gharama nafuu ambazo
zitakopeshwa kwa wanachgama wa mfuko huo.
ILALA, Dar es Salaam
Mfuko wa
Pensheni kwa Watumishi wa Umma (PSPF) umekamilisha awamu ya kwanza ya
ujenzi wa nyumba 641 katika mikoa mitano ambazo zilianza kuuzwa tangu
Novemba mwaka 2012. Mradi huo unalenga kutatua tatizo la makazi kwa
wanachama wake na jamii kwa ujumla.
Mikoa
iliyojengwa nyumba hizo na idadi ya nyumba katika mabano ni Dar es
salaam – Buyuni (491), Morogoro – Lukobe (25), Shinyanga – Ibadakuli
(50), Tabora – Usule (25) na Mkoa wa Mtwara – Mang’amba (50).
Aidha kwa Muji
wa maelezo ya Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa PSPF, Bwana Adam Mayingu
amewaambia wanaadishi wa habari na viongozi mbalimbali waliotembelea
eneo la mradi huo Mkoawa Dar es Salaam kuwa Shirika lake limejenga
nyumba za aina nne ambazo ni za nyumba viwili, Vyumba vitatu, Nyumba za
vyumba vitatu kimoja ikiwa ni Master na Nyumba ya vymba vine kimoja
kikiwa ni Master.
Gharama ya
ununuzu wa nyumba hizo ambazo zinauzwa kwa wanachama wa Mfuko huo ni
kati ya Shilingi Milioni 64 hadi milioni 94 gharama zikijumlishwa na
Kodi ya ongezejo la Thamani.
picha na habari kwa hisani ya mtandao wa francisdande.blogspot.com