Na Dina Ismail
WANACHAMA na mashabiki wa soka nchini wameapa kuandamana
na kwenda Mahakamani kuzuia kufanyika kwa uchaguzi wa viongozi wa Shirikisho la
soka Tanzania (TFF), baada ya Kamati ya Rufaa ya Shirikisho hilo kumuengua
mgombea wa nafasi ya urais, Jamal Emil Malinzi.
Aidha, wanachama
hao kutoka klabu za Simba, Yanga na Azam wamemtaka Rais wa Jamhuri ya Muungano
wa Tanzania, Jakaya Mrisho Kikwete kuingilia kati suala la kuenguliwa kwa
Malinzi kwani limefanywa kwa chuki binafsi likiwa na lengo la kumbemba mpinzani
wake, Athumani Jumanne Nyamlani.
Wakizungumza na Waandishi
wa habari leo, pamoja na kupinga kuondolewa kwa Malinzi, wametoa siku tatu kwa
TFF kumrejesha katika kinyang’anyiro hicho, kinyume na hapo watakwenda kudai
haki yao Mahakamani.
Mmoja ya wadau hao
Kaisi Edwin alisema kwamba kanuni za Shirikisho la Soka la Kimataifa (FIFA)
chombo cha mwisho cha maamuzi ni Mahakama yas Usuluhishi wa Migogoro ya Michezo
(CAS) lakini TFF haijaelekeza baada ya kamati ya Rufaa chombo kipi kinaweza kutoa
suluhu ya masuala kama hayo.
Alisema walitaka
kupata changamoto mpya ya uongozi kupitia kwa Malinzi lakiini kitendo cha
kumuengua kunaonesha ni jinsi gani wanavyotaka kuendelea kuwa na watu wasiotaka
maendeleo ya soka.
“Ni bora tufungiwe
na FIFA, tunajua maslahi wanayoyapata TFF na tutatoa uozo wote...kwa hili hata
damu itamwagika na kwa gharama yoyote tutahakikisha uchaguzi haufanyiki kama
wasipomrejesha Malinzi labda waende kufanyia Geneva,”aliusema Kaisi.
Naye Suleiman Kato
alisema anashangazwa na kamati ya Rufaa kumuengua Malinzi kwa madai ya kutokuwa
na uzoezfu wakati alipitishwa kugombea uchaguzi wa mwaka 2008 inagawa
alishindwa kwa kura chache na rais wa sasa wa TFF, Leodger Tenga.
“Malinzi pia nia mwenyekiti wa chama cha soka
Kagera sasa iweje apitishe kugombea huko na mpaka anapata kiti hicho nah ii leo
mseme hana uzoefu na uongozi wa soka, kinachoonekana hapa ni kutaka kudidimiza
soka la Tanzania, hilo hatulikubali,”alisema.
Mdau mwingine,
Mgeni Ramadhan ‘Dogo Macho’ alisema inaonesha wazi wazi wanataka viongozi kwa
ajili ya maslahi binafsi kitu ambacho si sahihi kwani Watanzania wanaopenda
soka wanataka maendeleo na si viongozi maslahi.
“Naamini Rais Kikwete
ambaye ni mpenda michezo atasikia kilio hiki na kuingilia kati, kuna watu wapo kwa
ajili ya kubebwa, huyo Nyamlani anatoka Kusini, kuna mwanakamati mmoja Murtaza
mangungu ambaye ni Mbunge anambeba, pia kuna mwingine aliwahi kuwa Hakimu wa
Temeke na nyamlani akiwa karani wake,”alisema.
Kwa upande wake,
mdau mwingine Said Bakari alisema kuwa wataanza kuonesha hasira zao kuanzia leo
kwenye uwanja wa Taifa kwenye mechi baina ya Yanga na African Lyon, kabla ya
kuendelea na hatua yao katika michezo ya kimataifa ya timu za Simba na Azam
wikiendi hii.
“Huyu Nyamlani
anabebwa, kwani tunajua Mwenyekiti wa Kamati alikuwa rafiki yake wakati akiwa
Hakimu Temeke yeye, alikuwa karani, Mangungu naye pamoja na kumpigia debe ni
jirani na baba yake Nyamlani,”alisema.
Wadau hao kwa
pamoja wamepaza sauti hizo baada kamati ya Rufaa ya TFF kumuengua Malinzi
katika uchaguzi huo unaotarajiwa kufanyika Februari 24 mwaka huu ambapo kwa
mujibu wa ratiba kampeni zinatarajiwa kuanza leo.
Katika hatua
nyingine, Malinzi kesho anatarajiwa kuzungunmza na waandishi wa habari kuhusina
na sakata hilo.Habari hii ni kwa mujibu wa mtandao wa Bin zuberi.
0 comments:
Post a Comment