Msanii wa maigizo hapa nchini ambaye kwa sasa anatamba katika muziki wa Ijili, Sarah Mvingi amesema kwamba uzinduzi wa albam yake iitwayo 'Asante Yesu' unatarajia kufanyika Mei 17 mwaka huu kwenye Ukumbi wa Diamond Jubilee jijini Dar es Salaam.
Akichonga na mtandao huu hivi karibuni, Sarah alisema kuwa pamoja na uzinduzi huo lakini kutakuwa na ziara maalum iliyopewa jina la 'Ukombozi Tour' ambayo itahusisha mikoa minne ya Tanzania Bara ambayo ni Dar es Salaam, Iringa, Tanga na Kilimanjaro yenye lengo la kusaidia watoto yatima, wazee na watu wenyeshida mbalimbali kitika jamii.
Na hii ndiyo kazi yenyewe hakikisha unapata nakala yako sasa!