Saturday, February 21, 2009

Sarah Mvungi kumshukuru Yesu Mei 17





Msanii wa maigizo hapa nchini ambaye kwa sasa anatamba katika muziki wa Ijili, Sarah Mvingi amesema kwamba uzinduzi wa albam yake iitwayo 'Asante Yesu' unatarajia kufanyika Mei 17 mwaka huu kwenye Ukumbi wa Diamond Jubilee jijini Dar es Salaam.

Akichonga na mtandao huu hivi karibuni, Sarah alisema kuwa pamoja na uzinduzi huo lakini kutakuwa na ziara maalum iliyopewa jina la 'Ukombozi Tour' ambayo itahusisha mikoa minne ya Tanzania Bara ambayo ni Dar es Salaam, Iringa, Tanga na Kilimanjaro yenye lengo la kusaidia watoto yatima, wazee na watu wenyeshida mbalimbali kitika jamii.


Na hii ndiyo kazi yenyewe hakikisha unapata nakala yako sasa!



8 comments:

Anonymous said...

Inamaana Hany ameamua kuachana na masuala ya kuigiza sasa yupo kwenye muziki.

Anonymous said...

Ane anauwezo mkubwa wa kuimba naamini kuwa hiyo siku mambo yaweza kuwa bomba mbaya.

Anonymous said...

Kama ameamua kuingia kwenye fani hii badi ni jambo la kumshukuru Mungu kwa maana namfahamu huyu dada kuwa alikuwa ni miongoni mwa wanadada mahiri na machachari katika masuala ya ulabu na ngono ila kwa hili jina la mwana lishukuriwe na kuhimidiwa milele.

wazalendomedia.com said...

ndugu yangu hanny hajaachana na maigizo ila kwa sasa ameelekeza nguvu zaidi kwenye muziki wa Injili ili kumtumikia Mungu.

Anonymous said...

Wewe mwenye wazalendo tuambie ukweli kwa maana tunajnua nje ndani ya msanii huyu au tuyaanike? unataka tufanye hivyo sema tunaweza kufanya ni mambo ambayo yahawezekana kufanyika tena bila tabu.

Anonymous said...

Kweli Mungu ni waajabu, mimi namfahamu Sara fika kwani tumekuwa naye hapa mkoani Tanga kwa muda mrefu ila katika suala hili aliloamua kumuimbia Mungu ni hatua big up mama utafika tu.

Anonymous said...

kazi uliyokuwa nayo Sara ni kubwa unatakiwa kumujomba Mungu ili kuweza kufikia katika kiwango cha mafanikio kala alichonacho Rose Mhando na Bahati Bukuku kwa maana licha ya kupata fedha lakini utakuwa umeifanya kazi ya Mungu kwa mafanilikio.

Anonymous said...

Kabla ya kuamua kufan ya hivyo lazima SARA atuhakikishie kwamba ambeachana na masuala yake ya tabia mbaya tulizokuwa tunazifahamu.