This is default featured slide 1 title

Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.

This is default featured slide 2 title

Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.

This is default featured slide 3 title

Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.

This is default featured slide 4 title

Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.

This is default featured slide 5 title

Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.

Friday, August 26, 2011

Baa La Njaa Somalia; Orodha Ya Waliochangia Na Jumla Iliyopatikana Hadi Sasa....




Watoto Wanne Wanakufa, Familia Moja; Tunafanya Nini?
Mwenzetu Bi. Naima Abdalah Besta amekuja na wazo la kuwachangia ndugu zetu wa Somalia na hususan watoto wanaokufa njaa kila siku. Na mchango wako waweza kuwa hata wa shilingi elfu moja. Na hapa ni taarifa ya michango hadi sasa;


1. Anonymous 100,000
2. Anonymous 100,000
3.Edwin Namnauka 15,000
4. Dennis Tagalile 20,000
5.Batamwa Rwamugila 5,000
6.Joyce Mpangile 5,000
7. Humphrey Mutakyawa 10,000
8. Dr. Bukaza Chachage 10, 000
9. Fidelis Msigwa 10,000
10.Sagisto Amon 24,500
11.Omari Mzirai 10,000
12. Anonimous 10,000
13. J. J Dickson 34,750
14. Priscula Mushi 30,000
15. David Kafulila 160,000
16. Salum Maleta 10,000
17. Zitto Kabwe 250,000
18. Ephraem Madembwe 10,000
19. Sarafina Hossa 10,000
20. Fullshangweblog 20,000
21. Chibiriti 20,000
22.Joseph Rwezahura 5,000
23. Joseph Ludovic 5,000
24.Godwin Mbwiga 21,000
25.Wenge Swill 5,000
26.Brown Mwashimaha 5,000
27. Mrisho Mpoto (Mjomba) 50,000
28. Ausy Francis 15,000
29. Sigisto Simba 29,750,00
30. Anonimous 155,622, 78
31. Anonimous 20,000
32. Hamisi Omari 10,000
33. Nelson Bisigoro 15,000

Jumla iliyopatikana hadi sasa ni; 1,200,622, 78 (Shilingi Milioni Moja, laki mbili na mia sita na ishirini na mbili na senti sabini na nane )

Bado tunaendelea kukusanya michango yenu...
Na hapa ni taarifa husika; Zaidi ya watu milioni 10 wanakabiliwa na baa la njaa katika nchi 3 za Afrika Mashariki. Watoto zaidi ya milioni mbili wako katika hali mbaya. Watoto laki 5 wamekumbwa na utapia mlo mbaya unaohatarisha maisha yao. Kati yao watoto zaidi ya 10 hufa kila siku.

Kwa mujibu wa taarifa za Shirika la Msalaba Mwekundu Duniani, shirika hilo linahitaji Dola za Kimarekani milioni themanini hadi kufikia mwisho wa mwaka huu ili liweze kufanikisha kazi ya kuokoa maisha ya ndugu zetu wa Somalia na hususan watoto.

Tulio tayari tusaidie kwa kuchangia kwa ajili ya watoto hao waliokumbwa na janga la njaa huko Somalia. Michango hiyo itakapopatikana itapelekwa moja kwa moja Red Cross Dar es Salaam ili baadae iwafikie walengwa.


Changia kwa kutuma kwa M-PESA 0754 678 252 Au TIGO PESA; 0712 95 61 31, ZAP 0788 111 765 ( Maggid Mjengwa) Au NMB- PESA-FASTA- 0754 678 252 ( Ukituma kwa NMB- PESA-FASTA unijulishe kwa ujumbe ili nipate nr ya simu ya mtumaji ambaye atakuwa na namba za siri za kutolea pesa)

Au ukitaka unaweza pia kutuma moja kwa moja kwenye Account Number:

01j2070759000 ( CRDB, Iringa) Jina, Maggid j. Mjengwa

Anayechangia kwa njia ya benki anijulishe kwa email au sms.
Au kwa Western Union, Maggid Mjengwa, Iringa. ( Atumaye anijulishe pia)


Namna nyingine rahisi ya kuchangia? Wasiliana na;


mjengwamaggid@gmail.com au sms; +255 754 678 252, Plus 255 712 95 61 31
Utapata maelezo ya njia rahisi ya kutuma mchango wako.

Mwisho wa kukusanya michango ni Septemba 11, 2011. Baada ya hapo tutaweka orodha ya majina na kiasi kilichochangwa kwenye Mjengwablog (http://mjengwa.blogspot.com/) na iwapo hutataka jina lako liwemo kwenye orodha, basi, utatambulika kama 'anonimous'.

Wahenga walinena; kutoa ni moyo, usambe ni utajiri.

Wenu,

Maggid Mjengwa

Mratibu wa Michango

Makamanda wa Bunge



Mbunge wa Temeke, Abbas Mtemvu (wa pili kulia) Mbunge wa Kigamboni Dk Faustine Ndugulile (wa kwanza kulia) na Mbunge wa Mbeya Mjini Joseph Mbilinyi a.k.a Mr. II, (Wa tatu kushoto) akiwa na baadhi ya wabunge wa kizazi kipya bungeni Dodoma leo.

Uuzwaji wa mahakama mazungumzo yaendelea



Na Veronica Kazimoto – MAELEZO

DAR ES SALAAM

Mazungumzo bado yanaendelea kati ya Serikali na Muwekezaji aliyejitokeza kununua jengo la Mahakama ya Rufani iliyopo katika makutano ya barabara ya Kivukoni na Ohio jijini Dar es Salaam.

Hayo yamesemwa na Waziri wa Katiba na Sheria, Mhe. Celina Kombani wakati akijibu hoja mbalimbali za wabunge waliokuwa wakichangia hotuba ya makadirio ya bajeti ya wizara hiyo.

“Kuhusu suala la uuzwaji wa jengo la Mahakama ya Rufani, mazungumzo baina ya Serikali na muwekezaji aliyejitokeza bado yanaendelea hivyo basi napenda kuwatoa hofu waheshimiwa wabunge kuhusiana na suala hili,” amesema waziri Kombani.

Waziri Kombani amefafanua kuwa mazungumzo yanaendelea baina ya muwekezaji na ofisi mbalimbali za Serikali kama ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Mahakama ya Rufani,Wizara ya Maliasili na Utalii, Wizara ya Katiba na Sheria na Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi.

Aidha, Waziri Kombani amesema muwekezaji aliyejitokeza ameahidi kujenga mahakama ya Rufani yenye hadhi kulingana na umuhimu waka kama mhimili mojawapo wa dola.
Kama muafaka utafikiwa kati ya muwekezaji na Serikali jengo hilo la Mahakama ya Rufani litajengwa maeneo ya mtaa wa Chimala mkabala na barabara ya Taasisi ya Saratani ya Ocean Road.

Hivi karibuni vyombo mbalimbali vya habari vimekuwa vikitoa taarifa kuhusiana na jengo la Mahakama ya Rufani kununuliwa na muwekezaji wa hoteli ya Kempinski na kuwa sehemu ya hoteli hiyo kwa ajili ya maegesho ya magari.

Thursday, August 25, 2011

Miss Tanzania wapata elimu ya M-PESA


Meneja Huduma wa Bidhaa za Vodacom, Elihuruma Ngowi akifafanua jambo juu ya huduma ya M Pesa kwa washiriki wa Shindano la Vodacom Miss Tanzania 2011 katika kambi yao iliyopo jumba la Vodacom jijini Dar es Salaam jana.


Afisa Utawala wa Huduma ya M Pesa kutoka Vodacom, Emmanuel Pallangyo akigawa viperushi vilivyo na maelezo ya namna huduma ya M Pesa kwa washiriki wa Shindano la Vodacom Miss Tanzania 2011 katika kambi yao iliyopo jumba la Vodacom jijini Dar es Salaam ಜನ.


Baadhi ya washiriki wa shindano la Vodacom Miss Tanzania 2011, wakijisajili katika huduma ya M Pesa baada ya kupata semina juu ya faida na umuhimu wa kuwa umejisajili katika huduma hiyo jana wakiwa Kambini katika Jumba la Vodacom Miss Tanzania.

Washiriki wa shindano la Vodacom Miss Tanzania 2011, wakipiga picha na mabaunsa waliovalia vazi la M Pesa “Super Man” baada ya warembo hao na wenzao kupata semina juu ya faida na umuhimu wa kuwa umejisajili katika huduma ya M Pesa jana wakiwa Kambini katika Jumba la Vodacom.


Monday, August 22, 2011

Rais Jakaya Kikwete Kwenye Futari Zanzibar


RAIS wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dk Jakaya Mrisho Kikwete na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzin Dk.Ali Mohamed Shein, wakijumuika katika Futari ilioandaliwa na Rais wa Tanzania Dk.Kikwete katika viwanja vya Ikulu Zanzibar.

Dereva Chezani Sebunga aliyekuwa akiendesha gari la Mbunge, Mussa Khamis Silima na kupata ajali eneo la Nzuguni, Dodoma , akiwa katika machela akiingizwa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili jana, akitokea mkoani Dodoma. Mke wa Mbunge Silima, Mwanaheri Fahari alifariki dunia katika ajali hiyo.
Mbunge mteule kutoka Baraza la Wawakilishi Zanzibar,Mussa Khamis Silima, ambaye alipata ajali juzi katika aneo la Nzuguni, Dodoma, akiwa katika machela baada ya kushushwa kwenye gari jana katika Hospitali ya Taifa Muhimbili, akitokea Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Dar es Salaam, alikoletwa na ndege kutoka Dodoma. Mke wake, Mwanaheri Fahari alifariki na dereva wao Chezani Sebunga alijeruhiwa kwenye ajali hiyo.

Friday, August 19, 2011

Grand Malt katika chupa mpya


Viongozi wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL) wakigonganisha chupa za Grand Malt katika uzinduzi wa kinywaji hicho leo. Kushoto ni Mkurugenzi wa Masoko wa TBL, David Minja, Meneja Mawasiliano na Uhusiano wa TBL, Editha Mushi, Meneja wa Grand Malt Consolata Adam na Meneja Masoko wa kinywaji hicho, Fimbo

Na Mwandishi Wetu Kinywaji kisicho na kilevi cha Grand Malt kinachotengenezwa na Kampuni ya Bia Tanzania (TBL) ambacho kimekuwa kikipatikana katika kopo, sasa kitapatikana pia katika chupa la mililita 330.

Kampuni ya Bia Tanzania (TBL) kupitia kinywaji chake cha Grand Malt imezindua chupa mpya ya aina yake yenye ujazo wa mililita 330 katika kiwanda chake cha Dar es Salaam leo.

Grand Malt imekuwa ikiuzwa kwenye kopo zenye ujazo wa mililita 330 lakini kuanzia jana, itapatikana pia kwenye chupa mpya itakayouzwa sh 1000 kwa chupa na sh 20,000 kwa katoni kwa bei ya reja reja. “Chupa hii mpya itaziba pengo katika soko na kukifanya kinywaji hiki kupatikana kwa urahisi,” alisema Mkurugenzi wa Masoko wa TBL David Minja huku akisisitiza kuwa kinwaji hicho bado kitapatikana kwenye kopo pia.

Alisema Grand Malt ilizinduliwa Aprili mwaka jana lakini kwa sasa ni kinywaji namba moja kisichokuwa na kilevi Tanzania. “Tunawashukuru sana wateja wetu na umma kwa ujumla kwa kukikubali kinywaji hiki na kukifanya kiwe namba moja. Tunawahakikishia kuwa kitakuwepo sokoni muda wote ili kuendelea kuwaburudisha watanzania,” alisema Minja.

“Tunapozindua kinywaji hiki leo, tunapenda kuwahakikishia wateja wetu kuwa kinywaji kitakachouzwa kwenye chupa ni sawa na kile ambacho kinauzwa kwenye kopo, ambacho kina vitamini na mchanganyiko wa maziwa ya aina yake,” alisema Minja. Meneja wa Grand Malt Consolata Adam alisema, “Grand Malt ilizinduliwa Tanzania mwaka jana na leo tunapozindua chupa hii mpya, tunawashukuru wateja wetu kwa kutuunga mkono.”

Alisema kinywaji hicho kimetokea kuwa bora kwa sababu ya ladha yake nzuri inayoifanya inyweke kirahisi kwa kuwa ina vitamini, laktosi yenye ladha nzuri, inayoitofautisha na malt zingine sokoni. “Kinywaji hiki kinawafaa wafanyakazi wenye shughuli nyingi lakini pia kinafaa kwa matumizi ya nyumbani, wafanyakazi wa usiku, wanafunzi, vikao vya kibiashara na sherehe nyinginezo,” alisema Consolata.

Alisema TBL itaendelea kukitangaza na kusambaza kinwaji hiki na kuhakikisha kinawafikia watanzania wengi zaidi popote walipo. (Habari kwa hisani ya Mjengwablogspot)




Sunday, August 7, 2011

Maj. General Silas ' Mti Mkavu' Mayunga Amefariki Dunia




Major General Silas Mayunga (Pichani kushoto) amefariki jana asubuhi katika hospitali ya Apollo - New Delhi
Wakuu taarifa za uhakika nilizopata kutoka nchini India kuwa mpiganaji wetu shupavu na kiongozi mwadirifu, Luteni Gerenali Silas Mayunga hatuko naye tena, amefariki leo katika hospitali ya Apollo New Delhi, India ambako alikuwa amelazwa tangu mwezi, Julai 2011.
Generali Mayunga atakumbukwa kwa mengi kwa jinsi alivyotumikia Taifa letu kwa utumishi uliotukuka, atakumbukwa daima kwa jinsi alivyoongoza mapambano ya vita vya Kagera kumng'oa Nduli Idd Amin.

Mwenyenzi Mungu ailaze roho yake mahali pema. RIP

ZIARA YA MKE WA RAIS WA BURUNDI DKT,DENISE NKURUNZIZA

Mwanafunzi Zainab Musa wa shule ya sekondari maalumu ya watoto yatima WAMA-NAKAYAMA inayoendeshwa na Taasisi ya WAMA iliopo Wilaya ya Rufiji mkoa wa Pwani akimuonyesha mazoezi ya vitendo katika maabara jinsi ya tofauti matumizi ya moto Mke wa Rais wa Burundi Dkt. Denise Mucumi Nkurunziza (kushoto aliyevaa nguo ya brown) akiwa na Mke wa Rais na Mwenyekiti wa Taasisi ya WAMA ,Mama Salma Kiwete.


Picha ya pamoja ya wake wa Marais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar Mama Mwanamwema Shein na Dkt, Denise Nkurunziza wa Burundi pamoja na baadhi ya viongozi wa taasisi mbalimbali za wanawake Zanzibar.
Mke wa Rais wa serikali ya mapinduzi Zanzaibar Mama Mwanamwema Shein (kulia) akimpatia zawadi mbalimbali Mke wa Rais wa Burundi Dkt, Denise Nkurunziza baada ya hafla ya futari katika Ikulu ya Zanzibar jana। Denise yupo katika ziara ya siku sita nchini .
Mke wa Rais wa Burundi Dkt, Denise Nkurunziza akisiliza maelezo kutoka kwa moja wa wataalam wa taasisi za Visiwani Zanzibar katika ziara yake visiwani humo.