Monday, August 22, 2011

Rais Jakaya Kikwete Kwenye Futari Zanzibar


RAIS wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dk Jakaya Mrisho Kikwete na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzin Dk.Ali Mohamed Shein, wakijumuika katika Futari ilioandaliwa na Rais wa Tanzania Dk.Kikwete katika viwanja vya Ikulu Zanzibar.

Dereva Chezani Sebunga aliyekuwa akiendesha gari la Mbunge, Mussa Khamis Silima na kupata ajali eneo la Nzuguni, Dodoma , akiwa katika machela akiingizwa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili jana, akitokea mkoani Dodoma. Mke wa Mbunge Silima, Mwanaheri Fahari alifariki dunia katika ajali hiyo.
Mbunge mteule kutoka Baraza la Wawakilishi Zanzibar,Mussa Khamis Silima, ambaye alipata ajali juzi katika aneo la Nzuguni, Dodoma, akiwa katika machela baada ya kushushwa kwenye gari jana katika Hospitali ya Taifa Muhimbili, akitokea Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Dar es Salaam, alikoletwa na ndege kutoka Dodoma. Mke wake, Mwanaheri Fahari alifariki na dereva wao Chezani Sebunga alijeruhiwa kwenye ajali hiyo.

0 comments: