Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal,
(wa pili kulia) akiwa mbele ya Kaburi la Rais wa zamani wa Zanzibar
Hayati Idris Abdulwakil, wakati alipozuru Kijiji cha Makunduchi Mkoa wa
Kusini Unguja juzi. Rais Wakil alifariki dunia mwaka 2001. Dk Bilal
alifika eneo hilo juzi katika ziara yake ya kuwatembelea wazee mbali
mbali mkoani humo, jana. (Desemba 24, 2012.
Makamu akiondoka katika kijiji hicho cha Makunduchi baada ya kuzulu Kaburi la Hayati, Abdulwakil, jana.
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal,
akisalimiana na Mzee Ali Khamis Abdallah (98) ambaye ni mmoja kati
waasisi 10, waliokaa pamoja na kuunganisha vyama vya
African Association na Shiraz Association na kuwa Chama cha Afro Shiraz
Party (ASP), wakati akiwa katika ziara yake ya kutembelea wazee, leo
nyumbani kwake Mbweni, mjini Unguja. Kulia ni mke wa Mzee Ali, Asha Ali
Ghulam Hussein.
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal,
akizungumza na Mzee Ali Khamis Abdallah (98) ambaye ni mmoja kati
waasisi 10, waliokaa pamoja na kuunganisha vyama vya
African Association na Shiraz Association na kuwa Chama cha Afro Shiraz
Party (ASP), wakati akiwa katika ziara yake ya kutembelea wazee, leo
nyumbani kwake Mbweni, mjini Unguja.
0 comments:
Post a Comment