(Watuhumiwa wa uvuvi haramu wakiwa Mahakamani picha kwa hisani ya Global Publishers)
Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam, leo imekubali kuwapa dhamana washitakiwa 37 kutoka nchi za China, Vietnam, Japan, Ufilipino na Kenya wanaokabiliwa na mashitaka ya uvuvi haramu katika eneo la bahari ya Tanzania.
Akitangaza uamuzi huo mahakamani hapo, Hakimu Mkazi wa mahakama hiyo Bi. Walyarwande Lema aliwaondolea pingamizi la dhamana na kuwataka washitakiwa hao kila kundi kufuatana na nchi kuwa na wadhamini wawili wanaotambulika na ubalozi wao na kitita cha dola za Kimarekani 25,000.
Mpaka tunaelekea mitamboni washitakiwa hao walikuwa wakihangaikia kutimiza masharti hayo.
Wednesday, July 22, 2009
'MABAHARIA' WA MAGUFULI WAPETA
6:52 PM
1 comment
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
1 comments:
hawa jamaa wametubia lakini je hawa wanaotuibia raslimali nyingine wanachukuliwa hatua gani?.
Post a Comment