Monday, February 6, 2012

Kutoka Bungeni Mjini Dodoma


Waziri wa Nishati na Madini William Ngeleja akijibu maswali ya wabunge kuhusu upatikanaji wa umeme wa uhakika nchini na uondoaji wa tatizo la mgawo wa umeme unaoendelea kwenye baadhi ya maeneo nchini na kufafanua kuwa serikali inaendelea na mikakati ya utekelezaji wa miradi mbalimbali ya utoaji wa huduma ya umeme katika maeneo yasiyo na huduma hiyo na kuimarisha uzalishaji wa umeme wa uhakika katika Gridi ya Taifa kupitia vyanzo mbalimbali.

Waziri na Afya na Ustawi wa Jamii Dkt. Hadji Mponda(kushoto) akizungumza jambo na Waziri Mkuu Mizengo Pinda (kulia)ndani ya ukumbi wa Bunge leo mjini Dodoma.

Mbunge wa Kigoma Kusini (NCCR –Mageuzi) David Kafulila akichangia bungen kuhusu namna bora ya ukusanyaji wa mapato kupitia kodi zinazotozwa kwenye makampuni ya simu nchini ili kuongeza mapato ya serikali leo mjini Dodoma.


Naibu spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Job Ndugay akitoa ufafanuzi wa hoja mbalimbali zilizowasilishwa na wabunge wakati wa kikao cha tano cha mkutano wa sita leo mjini Dodoma.
Naibu waziri wa Wizara ya Fedha Gregory Theu (kushoto) akizungumza jambo na Naibu waziri wa Wizara ya Kilimo, Chakula na Ushirika Christopher Chiza (kulia) nje ya ukumbi wa Bunge leo mjini Dodoma.
Waziri wa Fedha Mustapha Mkulo (kulia) akitoa ufafanuzi wa masuala mbalimbali kwa wabunge mara baada ya kumalizika kwa kikao cha tano cha mkutano wa sita leo mjini Dodoma.Kutoka kushoto ni mbunge wa Kigoma Kaskazini Zitto Kabwe na Davidi Kafulila (wa pili kutoka kushoto) kutoka Kigoma kusini. Picha na Aron Msigwa –MAELEZO.

0 comments: