Monday, February 6, 2012

Makamu Wa Rais Dk Gharib Bilal Ikulu Jijini Dar es Salaam Leo

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akipokea zawadi ya kitabu cha China kutoka kwa Balozi wa China nchini Tanzania, Liu Xinsheng, aliyefika ofisini kwake Ikulu Dar es Salaam leo Februari 6, 2012 kwa ajili ya kumuaga baada ya kumaliza muda wake nchini
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akizungumza na Balozi wa China nchini Tanzania, Liu Xinsheng, aliyefika ofisini kwake Ikulu Dar es Salaam leo Februari 6, 2012 kwa ajili ya kumuaga baada ya kumaliza muda wake nchini.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akizungumza na baadhi ya Mabalozi wateule wanaokwenda kufanya kazi nchi za nje walizopangiwa, wakati walipofika ofisini kwake Ikulu Dar es Salaam leo Februari 6, 2012 kwa ajili ya kumuaga kabla ya kwenda kuanza majukumu yao ya kikazi katika nchi walizopangiwa.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiwa katika picha ya pamoja kwa kumbukumbu na baadhi ya Mabalozi wateule baada ya kumaliza mazungumzo nao wakati walipofika ofisini kwake Ikulu jijini Dar es Salaam leo Februari 6, 2012 kwa ajili ya kumuaga kabla ya kuondoa kwenda kuanza majukumu yao ya kikazi katika nchi walizopangiwa. Picha na Muhidin Sufiani-Ofisi ya Makamu wa Rais

0 comments: