Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiteta jambo na Waziri Mkuu Mstaafu Edward Lowasa, wakati wakiwa katika sherehe za mkesha wa Maulid, zilizofanyika usiku wa kuamkia leo, jana usiku Februari 04, 2012, katika viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam.
Muumin wa dini ya kiislam kutoka Msikiti wa Suni Hanafi wa jijini Dar es Salaam, Muzamil Chaki, akiimba Qaswaida jukwaani kutoa burudani wakati wa mkesha wa sherehe za Mauilid zilizofanyika katika Viwanja vya Mnazi Mmoja jijini jana usiku Februari 04, 2012.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akipokea kadi ya mwanachama wa CHADEMA, Mshindo Kisike, aliyekuwa Katibu mkuu na mweka hazina wa chama hicho Kata ya Kibaha, aliyejiengua na kujiunga na CCM, wakati Makamu akimalizia ziara yake ya Mkoa wa Pwani Wilayani Kibaha, jana Februari 04, 2012.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisalimiana na Rais Mstaafu wa awamu ya pili, Ali Hassan Mwinyi, wakati alipowasili kwenye viwanja vya Mnazi Mmoja katika shambrashambra za mkesha wa sherehe za Maulid, jijini Dar es Salaam jana Februari 04, 2012 usiku.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal(katikati) Rais Mstaafu wa awamu ya pili, Ali Hassan Mwinyi na Waziri Mkuu Mstaafu, Edward Lowasa, wakiwa katika sherehe za mkesha wa Maulid, zilizofanyika usiku wa kuamkia leo, jana usiku Februari 04, 2012, katika viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam.Picha na Muhidin Sufiani-Ofisi ya Makamu Wa Rais
0 comments:
Post a Comment