Tuesday, July 31, 2012
Man Utd yachafuka fedha
7:02 PM
No comments
LONDON, England
KLABU ya Manchester
United, imeingia mkataba wa miaka saba na Kampuni ya kutengeneza magari ya
nchini Marekani ya General Motors ambao utaanza kufanya kazi rasmi katika msimu
wa mwaka 2014/15.
Mkurugenzi wa
biashara wa klabu ya Manchester United, Richard Arnold, alisema kuwa ni moja ya
mafanikio kupata mkataba wa muda mrefu ambao utakuwa na manufaa makubwa kwa
klabu.
“Hili ni jambo jema
kupata mkataba wa muda mrefu kiasi hiki. Tulikutana na Chevrolet kwa muda wa
wiki sita tu, lakini waliweza kufanya jambo kubwa kiasi hiki ambalo lina faida
kwa pande zote ambao utasaidia kuwafikia mashabiki wetu zaidi ya milioni 659
kote duniani.
Kwa upande wake,
Alan Batey, kutoka kampuni ya General
Motors kwa upande wa Marekani ya Kaskazini,
alisema kwamba wamefurahi kuunganisha watu duniani kwa kutumia Manchester ambapo bidhaa
yetu ya Chevrolet itafikia watu wengi zaidi.
“Kwa mwendo huu
naamini tunaweza kuwafikia mashabiki wengi zaidi, lakini pili bidhaa yetu
inaweza kuwafikia watu wengi zaidi duniani, tofauti na awali ambapo tusingeweza
kufika kutokana na sababu mbalimbali.
“Tunajua kwamba
chini ya uongozi wa Alex Ferguson tunaimani kubwa kwamba bidhaa yetu itawafikia
watu wengi kwa ukaribu zaidi,” alikaririwa bosi huyo.
Mkataba huo ni wa
kitita cha pauni milioni 210 ambazo ni zaidi ya Sh bilioni 525, ambao utafunika
wa sasa na Kampuni ya AON.
Kutokana na tangazo hilo, imefanya kuongezeka
kwa nguvu ya hisa kwenye soko la kimataifa la hisa la Marekani jambo litakalowezesha
kuvutia wanahisa wengi.
Aidha kiasi cha
pauni milioni 30 ndicho kitakachokuwa kinatolewa kwa mwaka kwa ajili ya
kuchapisha jezi za klabu hiyo kila msimu, ambapo sasa imevuka ule wa mabingwa
wa zamani wa Ulaya Barcelona Qatar Foundation, ambapo inatumia kiasi cha pauni
milioni 25 kwa mwaka kwa ajili ya machapisho ya jezi kila mwaka.
Mkataba wa sasa wa
Manchester United na AON (jezi mpya
pichani) unafikia kiasi cha pauni
milioni 20 kwa mwaka huku ule wa awali na AIG ulikuwa wa pauni milioni 14 kwa mwaka hali
inayoonekana kukua kwa mtaji kila mkataba na kampuni mpya.
Kutokana na mkataba huo huenda inaongeza nguvu kwenye
mikakati yake ya usajili ambayo imelenga kuwasajili, Robin van Persie kutoka Arsenal kwa dau la pauni milioni 15 huku Mbrazil
Lucas Moura (19) kutoka klabu ya Sao Paulo ya Brazil kwa gharama ya pauni
milioni 30.
Man United na jezi mpya.
Sunday, July 29, 2012
Wednesday, July 18, 2012
BREAKING NEEEEEWZ!!! BOT YA SEA GAL INAZAMA KLM CHACHE KUTOKA UNGUJA
6:19 PM
No comments
Habari
zilizoufikia mtandao huu wa www.sufianimafoto.blogspot.com, zinasema
kuwa Boti ya Sea Gal, inazama katika moja kisiwa kilicho karibu na
kilometa chache kutoka Kisiwa cha Unguja, hivi sasa tayari Boti tatu za
Kilimanjaro zimefika eneo la tukio kwa ajili ya kutoa msaada wa kuokoa
watu mahala hapo. Lakini habari zisizothibitihswa mpaka sasa zinasema
kuwa wengine kati ya waliopo eneo hilo wanasema kuwa boti hiyo inawaka
moto na wengine wakisema kuwa inazama.
MinistrIKULU:Rais Jakaya Kikwete Akutana na Mkuu wa madhehebu ya Shia Ismailia Duniani,H.H. Karim Aga Khan
5:49 PM
No comments
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akimsindikiza Mkuu wa madhehebu ya
Shia Ismailia duniani,H.H. Karim Aga Khan, wakati alipomkaribisha Ikulu
jijini Dar es salaam leo kwa mazungumzo na baadaye chakula cha mchana.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwa katika mazungumzo na
Mkuu wa madhehebu ya Shia Ismailia duniani,H.H. Karim Aga Khan, wakati
alipomkaribisha Ikulu jijini Dar es salaam leo kwa mazungumzo na baadaye
chakula cha mchana.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akipeana mikono na Mkuu wa
madhehebu ya Shia Ismailia duniani,H.H. Karim Aga Khan, wakati
alipomkaribisha Ikulu jijini Dar es salaam leo Julai 18, 2012 kwa
mazungumzo na baadaye chakula cha mchana.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akimlaki na Mkuu wa madhehebu ya
Shia Ismailia duniani,H.H. Karim Aga Khan, wakati alipomkaribisha Ikulu
jijini Dar es salaam leo kwa mazungumzo na baadaye chakula cha mchana.Picha na IKULU.
Thursday, July 5, 2012
MELI ZA IRANI KUFUTWA NCHINI?
8:34 PM
No comments
RAIS KIKWETE AONGOZA BAARZA LA MAWAZIRI DODOMA LEO
8:29 PM
No comments
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiongea jambo na baadhi ya mawaziri na viongozi waandamizi serikalini baada ya kuongoza kikao cha Baraza la Mawaziri leo July 5, 2012 katika ukumbi wa TAMISEMI Dodoma. |
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiongoza kikao cha Baraza la Mawaziri leo July 5, 2012 katika ukumbi wa TAMISEMI Dodoma.
PICHA KWA HISANI YA OFISI YA WAZIRI MKUU
|
WAKAZI 8000 WAFAIDIKA NA HUDUMA ZA BENKI YA DUNIA, MKOA WA RUKWA
8:27 PM
No comments
Diwani kata ya MWIMBI wilaya MPYA ya KALAMBO Mkoa wa Rukwa Leonard
Shalamwana (wa tatu kulia)akimuonesha Mkuu wa wilaya Moshi Mussa
Chang'a(wa tatu kushoto) chanzo cha Mradi wa maji utakaogharimu zaidi ya
shilingi milioni 158.3 na kunufaisha takribani wakazi 8,000. Mradi huo
unadhaminiwa na benki ya dunia, wananchi pamoja na mfuko wa maendeleo wa
jimbo la Kalambo. Wengine kutoka kushoto ni Mratibu wa Miradi ya TASAF
wilaya John Kiondo na Kaimu Mkurugenzi wilaya Sumbawanga Crispin Luanda.
NA RAMADHANI JUMA,
AFISA HABARI, SUMBAWANGA
WAKAZI wapatao 8,000 wa vijiji viwili vya Majengo na Mwimbi
katika Kata ya Mwimbi wilaya mpya ya Kalambo Mkoa wa Rukwa wanatarajia
kunufaika na mradi wa maji safi
unatekelezwa katika kata hiyo kwa gharama ya zaidi ya shilingi milioni 158.3.
Mradi huo unadhaminiwa na Benki ya Dunia iliyotoa zaidi ya
shilingi milioni 154.4, wakazi wa kata hiyo wamechangia shilingi 2,709,000 na
mfuko wa jimbo la Kalambo umetoa shilingi 1,200,000 ili kufanikisha mradi huo.
Akielezea mradi huo mbele ya Mkuu wa wilaya ya Kalambo Moshi
Mussa Chang’a, diwani wa Kata ya Mwimbi Leonard Shalamwana alisema kwa sasa
mradi huo uko katika hatua ya nne ambayo ni usambazaji wa maji katika vituo
vikuu.
Afisa Mtendaji wa Kata hiyo Mosses Nkinda alisema mradi huo
utaongeza upatikanaji wa maji kwa wakazi hao na kuongeza kasi ya maendeleo na
kukuza hali ya kiuchumi mara utakapokamilika.
Kwa upande wake, Mkuu wa wilaya hiyo Moshi Mussa Chang’a
alipongeza utekelezaji wa mradi huo na kuwataka viongozi wa kata hiyo
kuhakikisha kuwa unakamilika haraka ili wakazi hao waanze kunufaika nao kama ilivyokusudiwa.
WAZIRI MKUU MIZENGO PINDA NA BUNGENI LEO
8:24 PM
No comments
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akiteta na Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongokwenye viwanja vya Bunge Mjini Dodoma Julai 6, 2012.(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu) |
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akiteta na Mbunge wa Ludewa, Deo Filikunjombe kwenye viwanja vya Bunge Mjini Dodoma Julai 6, 2012.(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu) |
AJISHINDIA JENERETA YA VUMBUA HAZINA CHINI YA KIZIBO
8:21 PM
No comments
|
Meneja masoko wa
kampuni ya bia ya Serengeti bw Eben Sauli kushoto ampongeza salvatory
Herald baada ya kumkabidhi zawadi ya jenereta aliojishindia .
|
Monday, July 2, 2012
Uzalendo wawakimbiza Wataalamu Zanzibar
8:00 PM
No comments
Habari zote na Juma Mohammed, MAELEZO Zanzibar
Kukosekana kwa uzalendo na tama ya kipato kikubwa kumetajwa
kuwa sababu ya ya baadhi ya wananchi wataalam kuacha kazi Serikali ya Mapinduzi
Zanzibar na kukimbilia ughaibuni.
Akijibu swali katika Baraza la Wawakilishi, Waziri wa Nchi
Ofisi ya Rais Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Haji Omar Kheri alikiri kuwepo
kwa tatizo la wataalam wa kizalendo kuondoka nchini kwa kutafuta maslahi zaidi
nje ya nchi.
Katika swali la
msingi,. Mwakilishi wa Jimbo la Wawi
(CUF) Saleh Nassor Juma alitaka kujua sababu za wataalamu kuendelea kukimbia
nchini.
Mwakilishi huyo apamoja na Mwakilishi wa Salum Abdallah
Hamad (CUF) wa Matambwe, Rashid Seif Suleiman (CUF) wa Ziwani na Jaku Hashim
Ayoub wa Jimbo la Muyuni (CCM) wote walilalamika kuwa serikali inachangia
kuwatorosha wataalamu kwa kuwawekea mazingira mabaya ya utendaji kazi na malipo
duni.
“Naomba nikubaliane na wajumbe wa baraza la wawakilishi kuwa
nchi nyingi zilizopo kwa janga la sahara hukimbiwa sana na wataalamu wake hususan madaktari
wakiwemo pia maprofesa na wahadhiri licha ya kulipwa stahiki mbali mbali”
alisema waziri Kheri.
Waziri alisema Zanzibar
pia imekuwa ikikabiliwa na tatizo la kukimbiwa na wataalamu wake hasa kada ya
udaktari hospitali ambao wanakwenda nchi nyengine kupata maslahi mazuri zaidi.
Hata hivyo waziri huyo alisema miongoni mwa sababu
zinazosababisha wataalamu kukimbia ni ukosefu wa maslahi bora na vitendea kazi
lakini kubwa zaidi ni kukosa uzalendo.
“Serikali imekuwa ikifanya juhudi za kuimarisha maslahi ya
watumishi wake na kuanzia mwaka jana wataalamu mbali mbali walirekebishiwa
mishahara pamoja na posho wakiwemo madaktari lakini licha ya hilo kutokana na kukosekana uzalendo baadhi
ya madaktari wanaondoka” alilalamika waziri huyo.
Waziri Kheri aliwataka wajumbe wa baraza la wawakilishi
kusaidia katika juhudi za kuwashawishi wataalamu waliokuwepo nchini kupenda
nchi yao na
kuwatumikia wananchi huku serikali ikifanya juhudi za kuimarisha maslahi na
mazingira bora ya kazi.
MANJI AZUA 'BALAA' TFF, UCHAGUZI YANGA WAINGIA KIZA
7:25 PM
No comments
Manji anaondoka TFF, umati ukimsindikiza |
Sura za huzuni; wanachama wakisikitika nje ya ofisi za TFF |
Wanachama wakisikitikia pingamizi la Manji |
Ni huzuni tupu |
Hakuna anayufurahia |
Kila mtu ana hasira |
Yaani watu wamekasirika ile mbaya |
Hadi akina mama wana hasira pia |
Manji anatoka chumba cha mahojiano |
Anaziacha ofisi za TFF |
Anapotea |
Anawasalimu wazee |
Anajadiliana na wazee |
Umati unamsindikiza |
Anafunguliwa mlango wa gari lake |
Anaingia na kupotea |
Na Prince Akbar
MAMIA ya wanachama wa klabu ya Yanga ya Dar es Salaam, leo
wameandamana hadi makao makuu ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Ilala,
Jijini kupinga pingamizi alilowekewa mgombea Uenyekiti wa klabu hiyo katika
uchaguzi wa Julai 15, mwaka huu, Yussuf Manji.
Kamati ya Uchaguzi ya TFF, chini ya Mwenyekiti wake, Deo
Lyatto leo ilikuwa inapitia pingamizi mbili walizowekewa wagombea, Manji na Stanley
Kavela ‘Yono’ anayewania Umakamu Mwenyekiti.
Tangu saa nne asubuhi hadi saa nane mchana, Kamati hiyo
ilikuwa inamuhoji Manji ambaye hata alipotoka, ilielezwa alitakiwa kurejea
tena.
Manji alitoka mara mbili na kurejea kufuata vielelezo
alivyotakiwa kuwasilisha kuhusiana na pingamizi alilowekewa, ambalo vyanzo vinasema
ni zito.
Tangu asubuhi wanachama walikuwa ‘kibao’ nje ya Ofisi za
TFF, zilizopo ndani ya Uwanja wa Karume, Ilala, Dar es Salaam wakionyesha
hasira zao dhidi ya pingamizi hilo, ambalo aliloliweka anafanywa siri.
Wanachama walisikika wakisema kwamba kama Kamati ya Lyatto
itamuengua Manji basi hakuna haja ya uchaguzi.
Miongoni mwa waliokuwapo katika wanachama ni wazee wa klabu
hiyo, akina Ibrahim Akilimali, Dk Idrisa Katundu na wengineo, wakiwemo
wanachama maarufu.
Kuna kila dalili kwamba uamuzi wa kumuengua Manji katika
uchaguzi huo litakuwa jambo la hatari kwa klabu hiyo, kwani wanachama tayari
wamekwishajenga imani kubwa juu yake.
Manji mwenyewe alipotoka kwenye chumba cha mahojiano
alionekana asiye na furaha hali ambayo ilizidi kuwatia wasiwasi wanachama
kwamba huenda kikao hakikuwa kizuri kwake.
PICHA NA HABARI KWA ZINATOKA MTANDAO WA BIN ZUBERY
Subscribe to:
Posts (Atom)