This is default featured slide 1 title

Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.

This is default featured slide 2 title

Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.

This is default featured slide 3 title

Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.

This is default featured slide 4 title

Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.

This is default featured slide 5 title

Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.

Friday, February 22, 2013

WADAU WA PSPF WAONESHWA NYUMBA ZA MKOPO ZILIZOPO BUYUNI CHANIKA

 Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Pensheni kwa Watumishi wa Umma (PSPF), Adam Mayingu akizungumza na waandishi wa habari wakati wa ziara ya viongozi wa Manispaa ya Ilala pamoja na wadau wa mfuko huo walipotembelea mradi wa nyumba za ambazo zitakopeshwa kwa wanachama wake zilizopo Buyuni, Chanika nje kidogo ya Dar es Salaam jana. (Picha na Dande JR)

Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Pensheni kwa Watumishi wa Umma (PSPF), Adam Mayingu (wa tatu kulia) wakati wa ziara ya viongozi wa Manispaa ya Ilala pamoja na wadau wa mfuko huo walipotembelea mradi wa nyumba za PSPF zilizopo Buyuni, Chanika nje kidogo ya Dar es Salaam

Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Pensheni kwa Watumishi wa Umma (PSPF) Adam Mayingu (katikati) akiwaonesha maofisa wa Jeshi la Polisi moja ya nyumba 491 zilizopo katika mradi wa ujenzi wa nyumba za gharama nafuu ambazo zitakopeshwa kwa wanachgama wa mfuko huo.


ILALA, Dar es Salaam

Mfuko wa Pensheni kwa Watumishi wa Umma (PSPF) umekamilisha awamu ya kwanza ya ujenzi wa nyumba 641 katika mikoa mitano ambazo zilianza kuuzwa tangu Novemba mwaka 2012. Mradi huo unalenga kutatua tatizo la makazi kwa wanachama wake na jamii kwa ujumla.

Mikoa iliyojengwa nyumba hizo na idadi ya nyumba katika mabano ni Dar es salaam – Buyuni (491), Morogoro – Lukobe (25), Shinyanga – Ibadakuli (50), Tabora – Usule (25) na Mkoa wa Mtwara – Mang’amba (50).

Aidha kwa Muji wa maelezo ya Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa PSPF, Bwana Adam Mayingu amewaambia wanaadishi wa habari na viongozi mbalimbali waliotembelea eneo la mradi huo Mkoawa Dar es Salaam kuwa Shirika lake limejenga nyumba za aina nne ambazo ni za nyumba viwili, Vyumba vitatu, Nyumba za vyumba vitatu kimoja ikiwa ni Master na Nyumba ya vymba vine kimoja kikiwa ni Master.

Gharama ya ununuzu wa nyumba hizo ambazo zinauzwa kwa wanachama wa Mfuko huo ni kati ya Shilingi Milioni 64 hadi milioni 94 gharama zikijumlishwa na Kodi ya ongezejo la Thamani.
 
picha na habari kwa hisani ya mtandao wa francisdande.blogspot.com

Tuesday, February 12, 2013

UCHAGUZI MKUU WA TFF HATIHATI

Na Dina Ismail
 
WANACHAMA na  mashabiki wa soka nchini wameapa kuandamana na kwenda Mahakamani kuzuia kufanyika kwa uchaguzi wa viongozi wa Shirikisho la soka Tanzania (TFF), baada ya Kamati ya Rufaa ya Shirikisho hilo kumuengua mgombea wa nafasi ya urais, Jamal Emil Malinzi.
 
Aidha, wanachama hao kutoka klabu za Simba, Yanga na Azam wamemtaka Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Jakaya Mrisho Kikwete kuingilia kati suala la kuenguliwa kwa Malinzi kwani limefanywa kwa chuki binafsi likiwa na lengo la kumbemba mpinzani wake, Athumani Jumanne Nyamlani.
 
Wakizungumza na Waandishi wa habari leo, pamoja na kupinga kuondolewa kwa Malinzi, wametoa siku tatu kwa TFF kumrejesha katika kinyang’anyiro hicho, kinyume na hapo watakwenda kudai haki yao Mahakamani.
 
Mmoja ya wadau hao Kaisi Edwin alisema kwamba kanuni za Shirikisho la Soka la Kimataifa (FIFA) chombo cha mwisho cha maamuzi ni Mahakama yas Usuluhishi wa Migogoro ya Michezo (CAS) lakini TFF haijaelekeza baada ya kamati ya Rufaa chombo kipi kinaweza kutoa suluhu ya masuala kama hayo.
 
Alisema walitaka kupata changamoto mpya ya uongozi kupitia kwa Malinzi lakiini kitendo cha kumuengua kunaonesha ni jinsi gani wanavyotaka kuendelea kuwa na watu wasiotaka maendeleo ya soka.
 
“Ni bora tufungiwe na FIFA, tunajua maslahi wanayoyapata TFF na tutatoa uozo wote...kwa hili hata damu itamwagika na kwa gharama yoyote tutahakikisha uchaguzi haufanyiki kama wasipomrejesha Malinzi labda waende kufanyia Geneva,”aliusema Kaisi.
 
Naye Suleiman Kato alisema anashangazwa na kamati ya Rufaa kumuengua Malinzi kwa madai ya kutokuwa na uzoezfu wakati alipitishwa kugombea uchaguzi wa mwaka 2008 inagawa alishindwa kwa kura chache na rais wa sasa wa TFF, Leodger Tenga.
 
 “Malinzi pia nia mwenyekiti wa chama cha soka Kagera sasa iweje apitishe kugombea huko na mpaka anapata kiti hicho nah ii leo mseme hana uzoefu na uongozi wa soka, kinachoonekana hapa ni kutaka kudidimiza soka la Tanzania, hilo hatulikubali,”alisema.
 
Mdau mwingine, Mgeni Ramadhan ‘Dogo Macho’ alisema inaonesha wazi wazi wanataka viongozi kwa ajili ya maslahi binafsi kitu ambacho si sahihi kwani Watanzania wanaopenda soka wanataka maendeleo na si viongozi maslahi.
 
“Naamini Rais Kikwete ambaye ni mpenda michezo atasikia kilio hiki na kuingilia kati, kuna watu wapo kwa ajili ya kubebwa, huyo Nyamlani anatoka Kusini, kuna mwanakamati mmoja Murtaza mangungu ambaye ni Mbunge anambeba, pia kuna mwingine aliwahi kuwa Hakimu wa Temeke na nyamlani akiwa karani wake,”alisema.
 
Kwa upande wake, mdau mwingine Said Bakari alisema kuwa wataanza kuonesha hasira zao kuanzia leo kwenye uwanja wa Taifa kwenye mechi baina ya Yanga na African Lyon, kabla ya kuendelea na hatua yao katika michezo ya kimataifa ya timu za Simba na Azam wikiendi hii.
 
“Huyu Nyamlani anabebwa, kwani tunajua Mwenyekiti wa Kamati alikuwa rafiki yake wakati akiwa Hakimu Temeke yeye, alikuwa karani, Mangungu naye pamoja na kumpigia debe ni jirani na baba yake Nyamlani,”alisema.
 
Wadau hao kwa pamoja wamepaza sauti hizo baada kamati ya Rufaa ya TFF kumuengua Malinzi katika uchaguzi huo unaotarajiwa kufanyika Februari 24 mwaka huu ambapo kwa mujibu wa ratiba kampeni zinatarajiwa kuanza leo.
Katika hatua nyingine, Malinzi kesho anatarajiwa kuzungunmza na waandishi wa habari kuhusina na sakata hilo.

Habari hii ni kwa mujibu wa mtandao wa Bin zuberi.

Saturday, January 26, 2013

HALI TETE MTWARA: AMANI IMETOWEKA, SERIKALI LAWAMANI


Update:
Nyumba ya Mkuchika inawaka moto-Newala

Taarifa za redio mbao sasa  ni kwamba wananchi wanaendelea kufanya uharibifu mkubwa huko ambapo naambiwa wamevamia gereza wakafungulia wafungwa na kisha kupiga moto gereza. Polisi wamezidiwa na wamejifungia kituoni wanarusha mabomu yao tokea huko walikojificha maana nje hakutamaniki. Na wameshateketeza nyumba ya mama Anna Abdallah.

Update:
Kikao cha dharura cha kamati ya ulinzi na usalama kinaendelea kwa kuwashirikisha maafisa wa polisi na maafisa usalama waliotoka Dar es Salaam kuongezea nguvu.

Maaskari na makachero wawasili  Mtwara leo asubuhi na helkopta kuongezea nguvu.

Hosteli ya wanafunzi wa chuo cha Utumishi maeneo ya Kiyangu B Mtwara yakoswa koswa kuchomwa moto kwa kile kinachodhaniwa kuwa na uhusiano na Hawa Ghasia mpaka sasa wanafunzi hawana mahala pa kukaa.  Kituo kidogo cha Polisi Cha Shangani mkoani Mtwara nacho chakoswa na moto. Ofisi ya Afisa Mtendaji Nkanaledi mkoani Mtwara nayo yavunjwa.

Wananchi wamechoma moto mahakama ya Mwanzo na kuvunja vioo vya nyumba za waheshimiwa Hawa Ghasia (Waziri, TAMISEMI) na ya Mohamed Sinani (Mwenyekiti wa CCM Mkoa) zilizopo mtaa wa Sinani.


Wakiwa katika mahakama ya mwanzo, Polisi walizingirwa na vijana waliokuwa wamebeba mawe na kufunga barabara zote za kuingia na kutoka Kituo Kikuu cha Mabasi na eneo la Soko Kuu, licha ya kufyatua hewani mabomu ya machozi.

Baadhi ya barabara za zimezibwa kwa kuchomwa matairi ya gari, na kuongeza hofu kwa wananchi.

Hali imeshakuwa mbaya masasi taarifa zilizotufikia punde wamechoma eneo linaloitwa loliondo, ofisi za elimu na ofisi ya trafiki, inasemekana jamaa wameshavamia ofisi za halmashauri wengine wako njiani nyumbani kwa mama Ana Abdala, hapa Mtwara  mjini maduka yote eneo la soko kuu na stendi yamefungwa hakuna huduma, huko Newala , leo kuna mkutano mkubwa mchana huu wa kumkataa George Mkuchika.

Vurugu zahamia wilaya ya Masasi mkoani Mtwara Nyumba ya Mbunge wa Masasi nayo yateketezwa kwa Moto hivi sasa...Madereva Bodaboda waandamana ...Vurugu zashamiri Mabomu Kibao..Hali ni tete


POLISI jana  wamelazimika kupiga mabomu ya machozi kutwa nzima katika kata ya Chikongola, Manispaa ya Mtwara Mikindani kutawanya wananchi walioizingira nyumba ya diwani wa kata hiyo Mohamedi Chehako kwa madai ya kuwahifadhi wachawi ndani ya nyumba yake, huku mwandishi wa habari mmoja akiripotiwa kujeruhiwa.


Habari ambazo hazijathibitishwa na kamanda wa polisi mkoani hapa, Maria Nzuki zinadai kuwa majira ya saa 10 kasoro za jioni watu wanaodaiwa kuwa ni wanajeshi wa Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ) waliingilia kati na kuanza kutembeza mkong’oto kwa wananchi ili kuzima vuguvugu hilo.

Mwandishi wa habari hizi alipojaribu kuwasiliana na kamanda Nzuki kwa njia ya simu za mkononi hakuweza kupatikana.

Wananchi walitoa tuhuma hizo baada ya kukuta ungo ikiwa na tunguri ndani yake ambayo inadaiwa kuwa ni ndege ya wachawi uwanjani kwake maeneo ya makaburi Msafa.

Wananchi walijikusanya nyumbani kwa Diwani huyo na kumshinikiza awatoe wachawi nje ili waweze kuwadhibu, amri iliyopingwa na Diwani huyo. Kadiri mda ulivyokwenda ndivyo wananchi walivyozidi kuongezeka na hatimaye kulijitokeza kundi la watu walioanza kutia vurugu, hali iliyomlazimu Chehako kuomba msaada wa polisi.

Mashuhuda wa tukio walimweleza mwandishi wa habari hizi kuwa polisi walipofika waliwasihi wananchi kutawanyika kwa kuwa ungo na tunguri zake zilikuwa zimeteketezwa kwa moto na diwani huyo mbele ya wananchi hao.

Chehako akihojiwa nyumbani kwake alisema: “Wananchi waliendelea kupinga na kudai ndani ya nyumba kuna rubani na abiria wa ndege nimewahifadhi…polisi wakawachagua wananchi watano na kuingia ndani ya nyumba kuwasaka watu hao…hawakuona kitu, walitoka nje na kuwamabia wenzao hata hivyo wenzao walibisha.

Walianza kurusha mawe nyumba… polisi walianza kupambana nao kwa kuwarushia mabomu…hata hivyo wananchi walikuwa wanakimbia na kwenda upande wapili kufanya vurugu.”

Chehako alibainisha kuwa ni kawada yake kuamka alfajiri kwa ajili ya sala ya asubuhi, lakini asubuhi ya jana alishindwa kuamka mapema, hata hivyo hakuweza kuhisi jambo lolote: “Ilipofika saa 12 asubuhi nikaanza kusikia watu wakishangaa kitu nje, nilipotoka nikakuta nyungo na tunguri ndani yake…mara wakaja vijana wawili na pikipiki wakachukua ule ungo na kukimbia nao…nikawatuma vijana wawafuate waurudishe…walifanikiwa na nyungo ile ilirejeshwa nyumbani hapa na ndipo nilipouteketeza kwa moto.

Nilidhani yatakuwa yameisha, lakini wananchi waliendelea kudai nimewafungia wahuska ndani, si kweli hakuna mtu humu ndani wala mimi sijui kilichotokea hadi hivyo vitu vikawa humu ndani.”

Katika mapambano hayo ya wananchi na polisi, wananchi kwa kutumia mawe wamemjeruhi Mwandishi wa Habari wa Channel Ten mkoani hapa, John Kasembe kwa jiwe kichwani, sehemu za kisogoni ambapo ametibiwa zahanati ya Fajima na anaendelea vizuri.

Kwa mujibu wa Kasembe, alipigwa mawe kichwani akiwa kazini kukusanya habari na wananchi waliokuwa wakiwarushia mawe polisi.

Ofisa wa polisi ambaye jina lake hakutaka litajwe kwa sababu si msemaji wa jeshi hilo amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kuongeza kuwa gari moja ya polisi PT 1421 limevunjwa kioo cha mbele kwa mawe.

Hadi saa 10.00 jioni bado polisi walikuwa wanaendelea kupiga mabomu ya machozi hewani huku wananchi wakionekana kujipanga katika makundi hali iliyotishia usalama wa maeneo hayo.

Hii ni kwa mujibu wa www.mtwarakwetu.blogspot.com

Friday, January 25, 2013

mambo ya tuzo safi

Maandalizi ya tuzo za wazalendo 2012 yanaendelea vizuri ambapo kila kitu kinakwenda sawa.

Wednesday, December 26, 2012

Yaliyojiri X-MASS


Kikosi kazi cha SKYLIGHT Bendi kikiongozwa na Joniko Flower kuporomosha burudani mwishoni mwa juma katika kiota cha Thai Village Masaki jijini Dar es Salaam. USIKOSE Mkesha wa X-MASS na SKYLIGHT BAND leo Usiku kuanzia saa tatu pale pale Thai Village.
Diva's wa SKYLIGHT Band Aneth Kushaba AK 47 sambamba na Mary Lucos wakishambulia jukwaa.
SONY MASAMBA sambamba na Aneth Kushaba AK47 wakipiga shoo ya nguvu.
Muziki umenoga mpaka wengine waliamua kuvua mashati.
Pichani juu na chini ni Binti wa Kiafrika mrembo aliyeumbika kisawa sawa.... akimwaga radhi mbele ya kadamnasi kuonyesha umahiri wake wa kuzungusha nyonga wakati nyimbo ya Carolina ikiimbwa na kuwaacha hoi wengine wote waliokuwa kwenye dancing floor.
Sebene limekolea....asiyekuwa na mwana aeleke jiwe.
It's Reggae and Ragga time....Aneth Kushana AK 47 akionyesha ufundi wake.
Uzao wa BSS Mary Lucos akielekea kwenye viti kunyanyua mashabiki wake.
Mashabiki wa SKYLIGHT Band wakijimwaga kwa dancing floor.
Pichani Juu na Chini Umati wa Mashabiki wa SKYLIGHT Band wakizungusha mduara wa mbele aende mbele na wa nyuma arudi nyuma.
Pichani Juu na Chini ni Papa Justin Ndege na mdau wakiwatunza wapiga vyombo na waimbaji wa SKYLIGHT Bendi baada ya kuguswa na uimbaji pamoja na upigaji wa vyombo.
Mario Mpingirwa akionyesha jinsi gani anavyopenda kinywaji chake.
Papa Justine Ndege ( wa pili kulia) akiwa na marafiki wa karibu na mashabiki wa SKYLIGHT Bendi.
Wadau wa Makumbusho Kijitonyama, Yusuph (kushoto) huku Eric Ndalu akiwa na mai waifu.
Mdau Lussa ( wa pili kulia) alitia timu SKYLIGHT Band kula bata na marafiki zake.
One and Only Mekydiva Mash Macha (katikati) akishow love na Blogger King Kif, huku Jacqueline Mzindakaya akiipa mgongo Camera yetu.
Mdau Mwika (wa kwanza kulia) bila kukosa akishow love na marafiki zake.
Mashabiki nambari One wa Skylight Band wakishow love.
Models wakitega pozi kwa Kodak. Looking Fly Girls.
Hata shida na mtu kwa raha zake...Kuna msemo unasema 'raha jipe mwenyewe'.
King Kif na Mdau Godwin Gondwe a.k.a Double G alipita pande hizi kuchungulia burudani ya Sky Light Bendi ikoje.
Diva's wa SKYLIGHT Band Aneth Kushaba AK47 na Mary Lucos baada ya kupiga show ya nguvu walipata Ukodak.

Tuesday, December 25, 2012

MAKAMU WA RAIS DKT. BILAL AZURU KABURI LA HAYATI IDRIS ABDULWAKIL, MAKUNDUCHI, AMTEMEBELEA MZEE ALI KHAMIS ABDALLAH MUASISI WA AFRO SHIRAZ PARTY

 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, (wa pili kulia) akiwa mbele ya Kaburi la Rais wa zamani wa Zanzibar  Hayati Idris Abdulwakil, wakati alipozuru Kijiji cha Makunduchi Mkoa wa Kusini Unguja juzi. Rais  Wakil alifariki dunia mwaka 2001. Dk Bilal alifika  eneo hilo  juzi katika ziara yake ya kuwatembelea  wazee mbali mbali mkoani humo, jana.  (Desemba 24, 2012.
 Makamu akiondoka katika kijiji hicho cha Makunduchi baada ya kuzulu Kaburi la Hayati, Abdulwakil, jana.
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisalimiana na Mzee Ali Khamis Abdallah (98) ambaye ni mmoja kati waasisi  10,  waliokaa pamoja na  kuunganisha vyama vya African Association na Shiraz Association na kuwa Chama cha Afro Shiraz Party (ASP), wakati akiwa katika ziara yake ya kutembelea wazee, leo nyumbani kwake Mbweni, mjini Unguja. Kulia ni mke wa Mzee Ali, Asha Ali Ghulam Hussein. 
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akizungumza na Mzee Ali Khamis Abdallah (98) ambaye ni mmoja kati waasisi  10,  waliokaa pamoja na  kuunganisha vyama vya African Association na Shiraz Association na kuwa Chama cha Afro Shiraz Party (ASP), wakati akiwa katika ziara yake ya kutembelea wazee, leo nyumbani kwake Mbweni, mjini Unguja.

Tuzo za Wazalendo Januari 31



TUZO za Wazalendo 2012, zinatarajiwa kufanyika Januari 31 mwaka 2013 jijini Dar es Salaam badala ya Desemba 30 mwaka huu kama ilivyotangazwa hapo awali.

Mratibu wa tuzo hizo, Ahadi Kakore alisema kuwa kwamba sababu za kusogezwa mbele kwa fainali hizo ni kutoka Desemba 30 hadi Januari 31 ni kutokana na baadhi ya mambo kutokamilika kwa wakati, ingawa bado zitafanyika ndani ya jiji la Dar es Salaam.

Aidha sababu nyingine ni kwamba wanakamati wengi wamekuwa kwenye pilikapilika za uchaguzi wa Chama cha Makocha Tanzania (Tafca) kwa sababu wengi wao ni wanachama hivyo jambo ambalo limesababisha kushindwa kutekeleza baadhi ya mipango yao kwa wakati.

“Zipo sababu nyingi lakini kubwa ni kwamba baadhi ya wageni muhimu ambao walialikwa asilimia (80%) wameonyesha kutokuwepo kwa tarehe hiyo kwa sababu watakuwa nje ya jiji la Dar es Salaam kwa ajili ya siku kuu za mwisho wa mwaka.

“Kwa kuzingatia uzito wa jambo lenyewe kamati imeona ni busara kusogeza mbele kwa siku 30 kwa lengo la kuwapa nafasi wahusika kwa pande zote mbili kuendelea na matayarisho hayo,” alisema Kakore.

Katika hatua nyingine, majina ya wanasoka walioingia fainali ya tuzo za mwakasoka bora wa mwaka yanatarajiwa kuwekwa wazi Januari mosi mwaka huu baada ya kukamilishwa kwa mchakato wa kupitia majina 93 yaliyokuwa yamependekezwa na wadau wa soka.

Mchakato wa kumpata mwanasoka bora wa mwaka ulianza tangu Agosti mosi mwaka huu ambapo wadau mbalimbali wa ndani ya nje ya Tanzania walipendekeza majina ya wachezaji ambao walistahili kutwaa tuzo hiyo.


Tuzo za Wzalendo zinalenga katika kuinua na kutambua mchango wa maendeleo ya soka la Tanzania kwa kipindi cha mwaka wa 2012 ambapo zitakuwa zikifanyika kila mwaka lengo likiwa ni kuendeleza na kuthamini kazi ambazo zimefanywa na wanasoka na wadau wa soka kwa muda wa mwaka mmoja.

Tuesday, November 27, 2012

Dk Ali Shein katika ziara Vietnam



 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,(wa tatu kulia) akiwa na ujumbe wake wakipata maelezo walipotembela katika mabwawa ya ufugaji wa Samaki katika Chuo cha Uvuvi wa Samaki na ufugaji katika jimbo la Quang Ninh Mjini Halong nchini Vietnam,akiwa katika Ziara ya kiserikali
  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,alipowasili katika Chuo cha Uvuvi wa Samaki ikiwemo na ufugaji katika jimbo la Quang Ninh Mjini Halong nchini Vietnam,akiwa katika Ziara ya kiserikali.

 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,na ujumbe wake wakiwa na mazungumzo na Do Quang Sang,(kulia) Mkurugenzi pia Mwenyekiti wa Kampuni ya Bidhaa za Baharini,wakiwemo Samaki,Kamba pia usindikaji katika jimbo la Quang Ninh Mjini Halong nchini Vietnam,akiwa katika Ziara ya kiserikali
 Baadhi ya Viongozi wa Chuo cha Uvuvi wa Samaki ikiwemo na ufugaji katika jimbo la Quang Ninh Mjini Halong nchini Vietnam,wakiwa katika mkutano na ujumbe wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar,ukiongozwa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,katika ziara maalum ya Kiserikali nchini humo.
Balozi wa Tanzania nchini China ambae anawakilisha Vietnam Philip Sang’ka Marmo,(kutoka kushoto) Waziri wa Kilimo na Maliasili Suleiman Othman Nyanga,na Mshauri wa Rais Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Balozi Mohamed Ramia,wakiwa katika Mkutano na Uongozi wa Chuo cha Uvuvi wa Samaki na Ufugaji katika Jimbo la Quang Ninh Mjini Halong nchini Vietnam
 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,(kulia) akiangalia Samaki na Kamba waliokiwisha sindikwa ikiwa ni tayari kwa usafirishaji, alipotembelea katika kiwanda cha (Quang Ninh Sea Products Import Export Company) katika jimbo la Quang Ninh Mjini Halong nchini Vietnam,alipokuwa katika ziara ya Kiserikali,(kushoto) Mkurugenzi pia Mwenyekiti wa Kampuni kampuni hiyo, Do Quang Sang,(katikati) Nguyen Ha Dieu
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,akiagana na Do Quang Sang,Mwenyekiti pia Mkurugenzi wa Kampuni ya Import Export inayosindika na Bidhaa za Baharini katika Jimbo la Quang Ninh Mjini Halong Nchini Vietnam,baada ya kutembelea Kampuni hiyo,akiwa katika ziara ya Kiserikali.Picha na Ramadhan Othman,Ikulu-Zanzibar.

Chipukizi watesa Wazalendo awards 2012




KINYANG’ANYIRO cha kumpata mwanasoka bora wa mwaka 2012 katika tuzo za kila mwaka za Wazalendo, kimefikia pazuri baada ya majina ya wachezaji wachanga kuonekana kujitokeza zaidi ikilinganishwa na wale wenye umri mkubwa.

Mratibu wa tuzo hizo, Ahadi Kakore alisema kuwa tuzo za mwaka huu zimeonakana kuwa na msisimko mkubwa ambapo majina ya wachezaji wenye umri mdogo ndoyo yaliyopendekezwa zaidi ikilinganishwa na wakongwe.

“Tunafahamu kwamba kamati inaendelea na kazi yake ya kupembua majina lakini jambo kubwa lilionekana ni uwepo wa wachezaji wengi wachanga ikilinganishwa na wakongwe kitu ambacho kimeonekana kuwa ni cha tofauti.

“Ukiangalia uwiano yawachezaji wachanga na wakongwe ni dhahiri utaona kwamba kazi iliyopo  mbele ni kubwa katika kuhakikisha kuwa mambo yanakwenda sawa.

“Tunaimani kwamba angalau hadi kufikia tarehe za mwanzo za mwezi Desemba, tunaweza kujua mwelekeo kuwa nani ameingia na nani ameshindwa kuingia katika fainali.

“Kadhalika niwapongeze wote ambao wameendelea kutuunga mkono kwenye jambo hili kubwa katika maendeleo ya soka la Tanzania,” alisema Kakore.

Tunzo za Wazalendo zinatarajiwa kufanyika Desemba 30 mwaka huu jijini Dar es Salaam ambapo mshindi atapata tuzo, medali, cheti pamoja na fedha taslim.

R.I.P Sharo Milionea



Marehemu Sharomilionea enzi za uhai wake

Taarifa kuhusu kifo cha Msanii wa maigizo na Mziki wa Bongo fleva kufariki zimasamba nchi nzima masaa machache yaliopita.
Kwa mujibu wa chanzo cha habari ni kwamba amepata uthibitisho kutoka kwa diwani Makame Seif ambaye ni rafiki yake wa karibu sana wa Marehemu Hussen Ramadhani Mkiete maarufu kama Sharo Millionea amepata ajali mida ya saa mbili eneo la maguzoni Tanga na amefariki dunia papo hapo.

Polisi walitambua ni Sharo Millionea kwa vitambulisho vyake na picha moja ya passport aliokuwa nayo mfukoni ambavyo kwa sasa viko na polisi.
Diwani huyu alimfahamisha mwandishi kuwa Sharo Millionea aliumia vibaya sana kichwani, kifuani na kwenye mikono.
Pia Mjomba wa marehemu amethibitisha kuwa Sharo Millionea atazikwa Tanga na asubuhi ya leo ratiba ya msiba ingetolewa.
Ndugu na marafiki wa Sharo wameanza kwenda hospitalini baada tu ya taarifa hizi kuwafikia. Familia ya Sharo iliwasiliHospitali ya Teule ya Tanga mara baada ya kupata taarifa hizo.

 
Hii ndiyo gari aina Toyota Harrier yenye namba T278 BVR iliyopinduka na kusababisha ajali iliyopelekea kifo cha msanii Sharo milionea jana usiku mishale ya saa mbili.

Tuesday, November 20, 2012







HATUA ya utoaji wa tuzo za mwanasoka bora wa mwaka 2012, (Wazalendo Footballer of the Year)  imefikia patamu ambapo sasa fainali itafanyika Desemba 30 mwaka huu jijini Dar es Salaam.

Akizungumza jijini Dar es Salaam, Mratibu wa tuzo hizo, Ahadi Kakore  amesema kuwa tuzo za Wazalendo zitakua za tofauti lakini zikiwa na lengo la kusaidia maendeleo ya soka lakini pia suala la uchumi kwa wachezaji husika.

“Hadi sasa majina 93 yameshapigiwa kura na wadau wa soka ambapo kamati inahitaji majina 30 tu hivyo katika hatua hii vipio vigezo ambavyo vinaangaliwa kwa makini kabla ya kufanyika maamuzi ingawa mchakato wa kupitia majina unaendelea. 

“Pia utoaji huu wa tuzo utakwenda sambamba na kutoa elimu ya uwekezaji kwenye maeneo mbalimbali ya maendeleo ili kuongeza kipato cha wachezaji wetu ambaho kinaweza kuwasaidia hata baada ya kustaafu soka. Semina hiyo itafanyika Desemba 19 na 20 mwaka huu.

“Katika suala la afya, kamati itatumkia siku hizo mbili za semina ya uwekezaji kutoa elimu ya afya kwa wachezaji kwani afya ni jambo la kwanza kwenye michezo na uhai wa mwanadamu.

“Sababu ya kufanya semina hiyo  kwa wachezaji ni katika kuhakikisha kwamba  wachezaji wanapata maisha bora kwani wengi wa wachezaji wetu ni masikini jambo ambalo linawafanya kuendelea na hali hiyo hata baada ya kustaafu soka na baadhi yao kujikuta wanakuwa ombaomba wakati walifanya kazi kubwa kwa ajili ya nchi jambo ambalo si sahihi,” alisema Kakore.

Katika hatua nyiongine, Kakore alisema kuwa mshindi wa tuzo hiyo atapata tuzo, fedha taslim, medali na cheti. Licha ya kuwepo kwa tuzo hiyo ya mwanasoka bora lakini zitakuwepo nyingine tisa tofauti.