HATUA ya utoaji wa tuzo za mwanasoka bora wa mwaka 2012, (Wazalendo Footballer of the Year) imefikia patamu ambapo sasa fainali itafanyika Desemba 30 mwaka huu jijini Dar es Salaam.
Akizungumza jijini
Dar es Salaam,
Mratibu wa tuzo hizo, Ahadi Kakore
amesema kuwa tuzo za Wazalendo zitakua za tofauti lakini zikiwa na lengo
la kusaidia maendeleo ya soka lakini pia suala la uchumi kwa wachezaji husika.
“Hadi sasa majina
93 yameshapigiwa kura na wadau wa soka ambapo kamati inahitaji majina 30 tu
hivyo katika hatua hii vipio vigezo ambavyo vinaangaliwa kwa makini kabla ya
kufanyika maamuzi ingawa mchakato wa kupitia majina unaendelea.
“Pia utoaji huu
wa tuzo utakwenda sambamba na kutoa elimu ya uwekezaji kwenye maeneo mbalimbali
ya maendeleo ili kuongeza kipato cha wachezaji wetu ambaho kinaweza kuwasaidia
hata baada ya kustaafu soka. Semina hiyo itafanyika Desemba 19 na 20 mwaka huu.
“Katika suala la
afya, kamati itatumkia siku hizo mbili za semina ya uwekezaji kutoa elimu ya
afya kwa wachezaji kwani afya ni jambo la kwanza kwenye michezo na uhai wa
mwanadamu.
“Sababu ya
kufanya semina hiyo kwa wachezaji ni
katika kuhakikisha kwamba wachezaji
wanapata maisha bora kwani wengi wa wachezaji wetu ni masikini jambo ambalo
linawafanya kuendelea na hali hiyo hata baada ya kustaafu soka na baadhi yao
kujikuta wanakuwa ombaomba wakati walifanya kazi kubwa kwa ajili ya nchi jambo
ambalo si sahihi,” alisema Kakore.
Katika hatua
nyiongine, Kakore alisema kuwa mshindi wa tuzo hiyo atapata tuzo, fedha taslim,
medali na cheti. Licha ya kuwepo kwa tuzo hiyo ya mwanasoka bora lakini
zitakuwepo nyingine tisa tofauti.
0 comments:
Post a Comment