KINYANG’ANYIRO cha kumpata mwanasoka bora wa mwaka 2012 katika tuzo za
kila mwaka za Wazalendo, kimefikia pazuri baada ya majina ya wachezaji wachanga
kuonekana kujitokeza zaidi ikilinganishwa na wale wenye umri mkubwa.
Mratibu wa tuzo hizo, Ahadi Kakore alisema kuwa tuzo za mwaka huu
zimeonakana kuwa na msisimko mkubwa ambapo majina ya wachezaji wenye umri mdogo
ndoyo yaliyopendekezwa zaidi ikilinganishwa na wakongwe.
“Tunafahamu kwamba kamati inaendelea na kazi yake ya kupembua majina
lakini jambo kubwa lilionekana ni uwepo wa wachezaji wengi wachanga ikilinganishwa
na wakongwe kitu ambacho kimeonekana kuwa ni cha tofauti.
“Ukiangalia uwiano yawachezaji wachanga na wakongwe ni dhahiri utaona
kwamba kazi iliyopo mbele ni kubwa
katika kuhakikisha kuwa mambo yanakwenda sawa.
“Tunaimani kwamba angalau hadi kufikia tarehe za mwanzo za mwezi
Desemba, tunaweza kujua mwelekeo kuwa nani ameingia na nani ameshindwa kuingia
katika fainali.
“Kadhalika niwapongeze wote ambao wameendelea kutuunga mkono kwenye
jambo hili kubwa katika maendeleo ya soka la Tanzania,” alisema Kakore.
Tunzo za Wazalendo zinatarajiwa kufanyika Desemba 30 mwaka huu jijini
Dar es Salaam ambapo mshindi atapata tuzo, medali, cheti pamoja na fedha
taslim.
0 comments:
Post a Comment