Katibu Tawala wa Halmashauri ya wilaya ya Ukerewe Mariam Kaondo Mseleute
akimkabidhi kitita cha Tsh.700,000 Nahodha wa timu ya Sala wanawake,
Malgareth Selemani, kutoka eneo la Muruseni wilayani Ukerewe, baada ya
kuibuka mabingwa kwenye mashindano ya Mitumbwi (Balimi Boat Race) ngazi
ya Mkoa baada ya wilaya hiyo kupewa hadhi ya Mkoa kwa mashindano hayo
ambapo washiriki walishindana kuendesha mitumbwi kwa makasia.
Wasanii wa kikundi cha ngoma za asili cha Utandawazi wakiburudisha watu
waliohudhuria kwenye mashindano ya mitumbwi yaliyofanyika Wilayani
Ukerewe jana, ambapo washindi wa Wilaya hiyo iliyopewa hadhi ya Mkoa kwa
mashindano hayo watawakilisha wilaya hiyo kwenye fainali
zitakazofanyika mkoani Mwanza Disemba mbili mwaka huu.
Nahodha wa timu iliyoshika nafasi ya kwanza wanaume Bandiho Ignas akionyesha laki tisa.
Wasanii wa kikundi cha ngoma za asili cha Matwi Manene, wakitoa burudani
kwa wakazi wa Wilayani Ukerewe walioshudia mashindano ya mitumbwi ya
Balimi (Balimi Boat Race) yaliyofanyika Wilayani humo jana, ambapo
mitumbwi iliyoshinda itawakilisha wilaya hiyo iliyopewa hadhi ya ki mkoa
kwa mashindano hayo kwenye fainali za kanda zitakazofanyika Mkoani
Mwanza Disemba mbili mwaka huu.
Katibu Tawala wa Halmashauri ya wilaya ya Ukerewe Mariam Kaondo
Mseleute, akifungua mashindano ya mitumbwi ya Balimi ngazi ya mkoa
kutokana na Wilaya hiyo kupewa hadhi ya mkoa kwa mashindano hayo
yaliyofanyika jana Wilayani humo.
Kikundi vya wapiga makasia 15 wakinyosha makasia yao juu kabla ya kuanza
kwa fainali za mashindano ya mitumbwi ya Balimi (Balimi Boat Race) ngazi
ya Mkoa yaliyofanyika Wilayani Ukerewe jana kutokana na wilaya hiyo
kupewa hadhi ya Mkoa kwa mashindano hayo.
0 comments:
Post a Comment