Monday, November 12, 2012

Ushirikiano kati ya Tanzania na China wazidi kuimarika

 Kaimu Katibu Mkuu katika Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango, Bw. Longinus Rutasitara (katikati) akifafanua jambo wakati wa mkutano na Wajumbe kutoka Serikali ya Jamhuri ya Watu wa China na wadau wengine (hawapo pichani) kujadili misaada ya Serikali ya China katika kuisadia Tanzania kutekeleza miradi mikubwa katika sekta kama vile Kilimo, Miundombinu na Umeme. Wengine katika picha ni Maafisa Waandamizi kutoka Tume hiyo.
 
Balozi Mbelwa Kairuki (kulia), Mkurugenzi wa Idara ya Asia na Australasia katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa akitoa mchango wake wakati wa majadiliano na ujumbe kutoka Serikali ya China kuhusu kuisaidia Tanzania kutekeleza miradi yake mikubwa. Wengine katika picha ni Bw. Lin Zhiyong (katikati) Mwakilishi Mkuu katika masuala ya Uchumi na Biashara wa Serikali ya Jamhuri ya Watu wa China hapa nchini na Bi. Fang Wang, Afisa kutoka Ofisi hiyo.Picha na Habari-Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa

0 comments: