Tuesday, January 24, 2012

Fissoo:Wasanii Zijueni Sheria Za Filamu na Michezo Ya Kuigiza



Katibu Mtendaji wa Bodi ya Filamu Tanzania, Joyce Fissoo akionesha Sheria namba 4 ya mwaka 1976 ya Utengenezaji wa Filamu na Michezo ya Kuigiza kwa waandishi wa habari ambao hawapo pichani wakati akitoa ufafanuzi wa kuhusu sheria hyo kwa vyombo vya vya habari leo jijini Dares Salaam.
-----
Benjamin Sawe-Maelezo Dar es Salaam
Wasanii wa Filamu na Michezo ya Kuigiza wameshauriwa kuzisoma nyaraka mbalimbali za Bodi ya Filamu ili wajue sheria na kanuni zinazohusu tasnia ya hiyo.
Hayo yamesemwa leo jijini Dar es Salaam na Katibu Mtendaji wa Bodi ya Filamu nchini Joyce Fissoo alipokuwa akitoa ufafanuzi juu ya Sheria namba 4 ya Utengenezaji wa Filamu na Michezo ya Kuigiza ya mwaka 1976.

Akifafanua juu ya sheria hiyo, Bi Fissoo alisema ndiyo inayoendelea kutumika mpaka sasa na kukanusha tuhuma zilizosambazwa na baadhi ya vyombo vya habari kuwa ya uwepo wa matumizi ya sheria mpya.

“Hakuna Sheria mpya ya Filamu na Michezo ya Kuigiza iliyotungwa, Sheria inayoendelea kutumika ni ile ya mwaka 1976 bali kilichofanyika ni utekelezaji wa kanuni za sheria ya filamu na michezo ya kuigiza ambapo mchakato wake ulianza mwaka 2011.

Akizungumzia juu ya malalamiko ya baadhi ya wasanii kushindwa kuhimili kulipa ada ya Sh. 500,000(laki tano) Bi. Fissoo alisema kifungu cha 8 cha sheria hiyo kinampa Waziri mwenye dhamana husika kutoa msamaha wa malipo kwa msanii mchanga atakayeshindwa kulipa kiasi cha fedha hizo.

“Ada wanayolipa wasanii ya Sh.500, 000 (laki tano) ipo toka siku za nyuma ambapo Sheria namba 4 ya Filamu na Michezo ya kuigiza inampa mamlaka Waziri husika kutoa msamaha kwa msanii mchanga atakayeshindwa kulipa ada hiyo”.alifafanua.

Alisema kwamba msamaha wa ada ya sh. 500,000 utatatolewa pale tu msanii atakapotoa taarifa kwa Waziri husika na mara baada ya kujiridhisha ndipo msamaha utatolewa na kutangazwa kwenye gazeti la Serikali.

Amewashauri wasanii wa Filamu kuwa Wazalendo kwa kutengeneza filamu zenye maadili ya Mtanzania na si kutengeneza Filamu zenye maudhui ya kimagharibi.

0 comments: