Na Mwandishi Wetu
UONGOZI wa
Klabu ya Simba umesisitiza kuwa hauna mpango wa kumtema beki wa klabu hiyo,
Nassor Said ‘Cholo’ pamoja na Wilbert Mweta katika usajili ujao wa Ligi Kuu ya
Tanzania Bara.
Msemaji wa
Simba, Ezekiel Kamwaga amesema Simba wachezaji hao hawapo kwenye orodha wa wale
watakaotemwa katika usajili wa Ligi Kuu
Tanzania Bara msimu ujao.
“Simba ina
mipango mingi lakini katika usajili wake hatutawaacha nyota hao kama ambavyo
wengi wanavyoamini kwa sababu hawapo kwenye orodha ya wale wataoachwa.
“Kama kuna
taarifa za majeruhi ni suala la ndani ya
Simba na si busara kuliweka wazi, ila ninachosisitiza nikiwa ni kiongozi wa
Simba kwamba Cholo na Mweta wataendela kuwepo klabuni msimu ujao wa ligi.
“Pia wakati
wa kuwaacha wachezaji kwa ajili ya msimu ujao bado hivyo kauli za sasa kuwa
tunamuwacha fulani na fulani anabakia si taarifa kutoka ndani ya Simba ambazo
tunaziona kuwa na malengo mabaya na klabu yetu.
“Tunasema si
sahihi kwa sababu wapo baadhi ya wachezaji waliomaliza mkataba na Simba lakini
kutokana na umuhimu wao yapo mazungumzo yanayoendelea baina ya pande mbili
hizi.
“Nichukue
nafasi hii kuwasihi wanachana na wapenzi wa Simba kuwa makini katika wakati huu
na wasiyumbishwe bali wasubiri taarifa rasmi itatolewa na uongozi,” alisema
Kamwaga.
Cholo
aloijiunga na Simba akitokea JKT Oljoro ya Arusha katika usajili wa ligi kuu
msimu uliopita huku, Mweta akitua akitokea Toto Africans ya jijini Mwanza.
Pamoja na usajili huo, Cholo ndiye aliyepata nafasi kubwa ya kucheza zaidi ya
Mweta ambaye hakupata nafasi kutokana na uwepo wa kipa namba moja Juma Kaseja.
0 comments:
Post a Comment