Sunday, June 17, 2012

MWILI WA MAREHEMU WILLY EDWARD UKITOLEWA WASAFIRISHWA KWENDA DAR


Kaka mkubwa wa marehemu aliyekuwa Mhariri Mkuu wa gazeti la Jambo Leo, Willy Edward
Ogunde, George Ongiri Ogunde (wa kwanza kulia) akishirikiana na ndugu, jamaa na waandishi wa habari, kubeba mwili wa mhariri huyo, aliyefariki dunia ghafla jana usiku eneo la Forest Hill, mjini Morogoro. Mwili huo ulikuwa unatolewa chumba cha kuhifadhia maiti Hospitali ya Rufaa ya mkoa wa Morogoro kwa ajili ya kusafirishwa kwenda jijini Dar es Salaam kwa maandalizi ya mazishi katika Kijiji cha Mugumu kilichopo wilaya ya Serengeti, mkoani, Mara.. (PICHA ZOTE NA JUMA MTANDA BLOG)
Mbunge wa Jimbo la Morogoro, Azizi Abood, akiwa na Ofisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya New Habari (2006), Husein Bashe wakisubiri kuuona mwili wa Willy Edward
Baadhi ya waandishi wa habari akiwemo Mbunge wa Morogoro mjini, Azizi Abood, wakiwa na huzuni walipokuwa wakisubiri kutoa heshima za mwisho katika Hospitali ya Rufaa ya Morogoro, muda mfiupi kabla ya mwili kusafishwa Dar es Salaam.
Mkuu wa mkoa wa Morogoro, Joel Bendera (kulia) akisikiliza jambo kutoka kwa kaka mkubwa wa
marehemu aliyekuwa mhariri mkuu wa gazeti la Jambo Leo, Willy Edward Ogunde, George Ongiri
Ogunde muda mfupi kabla ya kuanza safari ya kwenda jijini Dar es Salaam kwa maandalizi ya mazishi katika kijiji cha cha Mgumo kilichopo wilaya ya Serengeti mkoani Musoma. wa pili kutoka kulia ni Katibu Tawala wilaya ya Morogoro, Alfred Shao na kaka mkubwa upande wa baba, Isack Ugunde.

0 comments: