Taarifa kutoka Shirikisho la soka Tanzania (TFF)
MSEMAJI WA TFF-BONIFACE WAMBURA
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI Juni 3, 2012
STARS YAJIPANGA KUIKABILI GAMBIA
Kikosi
cha Taifa Stars ambacho jana kilicheza na Ivory Coast hapa Abidjan na
kupoteza kwa mabao 2-0 kinaendelea kujinoa kwa mechi ijayo dhidi ya
Gambia itakayochezwa Jumapili (Juni 10 mwaka huu) Uwanja wa Taifa, Dar
es Salaam.
Kwa
mujibu wa programu ya Kocha Kim Poulsen, Taifa Stars imefanya mazoezi
leo asubuhi kwenye uwanja wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Ivory Coast
(FIF) ambao uko pembezoni mwa jiji la Abidjan.
Timu
hiyo itafanya tena mazoezi kesho (Juni 4 mwaka huu) asubuhi kabla ya
kuanza safari ya kurejea nyumbani saa 1.30 usiku kwa ndege ya Kenya
Airways kupitia Nairobi ambapo itawasili Dar es Salaam, Juni 5 mwaka huu
saa 1.40 asubuhi.
Kocha
Kim ambaye amekuja na wachezaji wote hapa ukiondoa wanne ambao ni
majeruhi (Thomas Ulimwengu, Nurdin Bakari, Haruna Moshi na Nassoro
Masoud Cholo) amesema hivi sasa wameelekeza akili yao kwenye mechi ijayo
dhidi ya Gambia.
“Safari
ya kujenga timu ndiyo imeanza. Mechi dhidi ya Ivory Coast imepita na
ninawashukuru wachezaji kwa kucheza kwa mujibu wa maelekezo na kujituma.
Mpira ni mchezo wa makosa, tumefanya makosa yaliyosababisha tuwape
Ivory Coast mabao mepesi.
“Lakini
kama nilivyosema mechi hiyo imepita, hivi sasa tunaangalia mechi ijayo
dhidi ya Gambia. Hatuna muda mwingine wa kujipanga na ndio maana
niliamua kuja na wachezaji wote Abidjan,” amesema Kim.
Mechi
dhidi ya Gambia itachezwa Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam kuanzia saa 10
jioni. Gambia ilitoka sare ya bao 1-1 na Morocco katika mechi
iliyochezwa juzi jijini Banjul.
Hata
hivyo, Taifa Stars haitakuwa na nahodha wake msaidizi Aggrey Morris
ambaye alionesha kadi nyekundu dakika ya 65 baada ya kupata ya pili ya
njano kwenye mechi dhidi ya Ivory Coast iliyochezwa Uwanja wa Felix
Houphouet-Boigny jijini Abidja.
0 comments:
Post a Comment