Aliyekuwa shambuliaji nyota wa kikosi cha Yanga B, Atupele
Green amejiunga na klabu ya Coastal Union kwa mkataba wa miaka mitatu
ikiwa ni maandalizi ya Ligi Kuu Tanzania
Bara.
Akizungumza na Smtandao huu, Green alisema kuwa amevutiwa na dau
alilopewa na Coastal ambapo ameongeza kuwa anaimani kuwa atapata nafasi ya
kucheza zaidi tofauti na klabu nyingine.
Kadhalika amefafanua kwmaba hana mpango na kucheza katika
klabu za Simba wala Yanga kwani anachikiangalia kwa sasa ni kucheza soka la
kulipwa.
“Nimeona kwamba hapa ndipo patakapokuw ana maisha bora ya
baadaye kwenye soka langu, imani yangu ni kwmaba nitaweza kupata mafanikio
makubwa katika siku zijazo hivyo sina shaka.
“Nihitaji kucheza soka kwa muda mrefu zaidi ambapo ili
kufanya hivi ni lazimia kwenye klabu ninatakayopata nafasi ya kutumika.
“Ninachikiamini ni kwamba, nataka kufanya kazi kubwa kwa
ajili ya nchi hii ninaangalia namna bora ya kuweza kutangaza jina langu na nchi
yangu hivyo hapa Coastal ndiyo nimeona panaweza kunifaa ndiyo maana nimekubali
kuja.
“Pia nimepewa dau nililokuwa nalihitaji kwa kama nilivyokuwa
nimepanga akilini mwangu,” alisema Green ambaye aliitumikia Yanga miaka mitano.
Katika hatua nyingine nyota huyo amesisitiza kuwa baada ya
mkataba wake kumalika ataangalia kucheza soka la kulipwa nje ya nchi na
hatakuwa na mpango wa kucheza kwenye Ligi kuu ya Tanzania Bara.
Awali Green alikuwa asajiliwe na Yanga lakini ilitokea hali
ya kutoelewana baina ya pande hizo mbili hali iliyofanya mkataba uliyokuwa
umeandaliwa kwa ajili yake kuchanwa hadharani.
0 comments:
Post a Comment