Ezekiel Kamwaga msemaji wa Simba
Na Mwandishi
Wetu
KLABU ya
Simba imelegeza msimamo wake baada ya kusema kuwa dau la sh bilioni mbili
iliyokuwa imetangaza awali kwa klabu inayotaka kumsajili mshambualiaji wake,
Emmanuel Okwi kuwa linaweza kupungua au kuongezekana.
Akizungumza
na tanzaniacelebrity.com msemaji wa Simba, Ezekiel Kamwaga alisema kuwa Simba
itakuwa tayari kufanya mazungumzo juu ya dau halisi la nyota huyo ambapo dau
hilo litategemea klabu inayomuita inaweza kutoa kiasi gani cha fedha.
Kwa sasa
Okwi ameitwa katika majaribo nchini Afrika Kusini katika klabu ya Orlando
Pirates ambapo kama akifuzu ndiyo mazungumzo ya uhamisho wake yatafanyika.
“Tupo tayari kumwachia kwa dau
tutakalokubaliana lakini kwa hivi sasa tunachoangalia ni kumsaidia kwa hali na
mali ili aweze kwenda na kufuzu majaribio yake kwani itakuwa ni sehemu muhimu
ya kuitangaza klabu yetu.
“Ni kweli awali tulitangaza dau hilo lakini
kwa sasa tunasubiri kwanza kama atafuzu ndiyo tutakuwa kwenye wakatiu mzuri wa
kujua anasajiliwa kwa kikasi gani kwa sababu
itategemea klabu inaweza kutoa kiasi gani.
“Kimsingi kama unavyojua katika usajili huwa
kunakuwa na mambo mengi lakini imani nyetu ni kwamba Simba inaweza kumuachia
Okwi kwa dau lolote kwa kuwa linaweza kuongezeka au kupungua,” alisema Kamwaga.
Awali Simba
ilitangaza kumuachia Okwi kwa dau la sh bilioni mbili kwa klabu ambayo ilikuwa
inahitaji kumsajili nyota huyo ambaye ameonyesha kiwango cha juu katika msimu
wa uliopita.
Tayari klabu
ya Orlando ya Afrika Kusini imeonekana kumhitaji mshambuliaji huyo mwepesi
kwenye kikosi chake kwa ajili ya Ligi Kuu ya Afrika Kusini.
Kabla ya kutua
Simba, Okwi alikuwa akiitumikia klabu ya SC Villa tangu mwaka 2009 ambapo
alifanikiwa kuifungia timu hiyo mabao 13 katika mechi 40 alizocheza. Hadi sasa
ameipa Simba mabao 17 kati ya mechi 27
alizocheza tangu mwaka 2010 alipojiunga na mabingwa hao wa Ligi ya Tanzania
Bara.
0 comments:
Post a Comment