Monday, November 12, 2012

Balimi Boat Race yakamilika Ukerewe

 Katibu Tawala wa Halmashauri ya wilaya ya Ukerewe Mariam Kaondo Mseleute akimkabidhi kitita cha Tsh.700,000 Nahodha wa timu ya Sala wanawake, Malgareth Selemani, kutoka eneo la Muruseni wilayani Ukerewe, baada ya kuibuka mabingwa kwenye mashindano ya Mitumbwi  (Balimi Boat Race) ngazi ya Mkoa baada ya wilaya hiyo kupewa hadhi ya Mkoa kwa mashindano hayo ambapo washiriki walishindana kuendesha  mitumbwi kwa makasia.
 
 Wasanii wa kikundi cha ngoma za asili cha Utandawazi wakiburudisha watu waliohudhuria kwenye mashindano ya mitumbwi yaliyofanyika Wilayani Ukerewe jana, ambapo washindi wa Wilaya hiyo iliyopewa hadhi ya Mkoa kwa mashindano hayo watawakilisha wilaya hiyo kwenye fainali zitakazofanyika mkoani Mwanza Disemba mbili mwaka huu.
 
Nahodha wa timu iliyoshika nafasi ya kwanza wanaume Bandiho Ignas akionyesha laki tisa.
 
Wasanii wa kikundi cha ngoma za asili cha Matwi Manene, wakitoa burudani kwa wakazi wa Wilayani Ukerewe walioshudia mashindano ya mitumbwi ya Balimi (Balimi Boat Race) yaliyofanyika Wilayani humo jana, ambapo mitumbwi iliyoshinda itawakilisha wilaya hiyo iliyopewa hadhi ya ki mkoa kwa mashindano hayo kwenye fainali za kanda zitakazofanyika Mkoani Mwanza Disemba mbili mwaka huu. 
 
Katibu Tawala wa Halmashauri ya wilaya ya Ukerewe Mariam Kaondo Mseleute, akifungua mashindano ya mitumbwi ya Balimi ngazi ya mkoa kutokana na Wilaya hiyo kupewa hadhi ya mkoa kwa mashindano hayo yaliyofanyika jana Wilayani humo. 
 
 Kikundi vya wapiga makasia 15 wakinyosha makasia yao juu kabla ya kuanza kwa fainali za mashindano ya mitumbwi ya Balimi (Balimi Boat Race) ngazi ya Mkoa yaliyofanyika Wilayani Ukerewe jana kutokana na wilaya hiyo kupewa hadhi ya Mkoa kwa mashindano hayo.

0 comments: