Tuesday, November 20, 2012







HATUA ya utoaji wa tuzo za mwanasoka bora wa mwaka 2012, (Wazalendo Footballer of the Year)  imefikia patamu ambapo sasa fainali itafanyika Desemba 30 mwaka huu jijini Dar es Salaam.

Akizungumza jijini Dar es Salaam, Mratibu wa tuzo hizo, Ahadi Kakore  amesema kuwa tuzo za Wazalendo zitakua za tofauti lakini zikiwa na lengo la kusaidia maendeleo ya soka lakini pia suala la uchumi kwa wachezaji husika.

“Hadi sasa majina 93 yameshapigiwa kura na wadau wa soka ambapo kamati inahitaji majina 30 tu hivyo katika hatua hii vipio vigezo ambavyo vinaangaliwa kwa makini kabla ya kufanyika maamuzi ingawa mchakato wa kupitia majina unaendelea. 

“Pia utoaji huu wa tuzo utakwenda sambamba na kutoa elimu ya uwekezaji kwenye maeneo mbalimbali ya maendeleo ili kuongeza kipato cha wachezaji wetu ambaho kinaweza kuwasaidia hata baada ya kustaafu soka. Semina hiyo itafanyika Desemba 19 na 20 mwaka huu.

“Katika suala la afya, kamati itatumkia siku hizo mbili za semina ya uwekezaji kutoa elimu ya afya kwa wachezaji kwani afya ni jambo la kwanza kwenye michezo na uhai wa mwanadamu.

“Sababu ya kufanya semina hiyo  kwa wachezaji ni katika kuhakikisha kwamba  wachezaji wanapata maisha bora kwani wengi wa wachezaji wetu ni masikini jambo ambalo linawafanya kuendelea na hali hiyo hata baada ya kustaafu soka na baadhi yao kujikuta wanakuwa ombaomba wakati walifanya kazi kubwa kwa ajili ya nchi jambo ambalo si sahihi,” alisema Kakore.

Katika hatua nyiongine, Kakore alisema kuwa mshindi wa tuzo hiyo atapata tuzo, fedha taslim, medali na cheti. Licha ya kuwepo kwa tuzo hiyo ya mwanasoka bora lakini zitakuwepo nyingine tisa tofauti.

0 comments: