Ligi kuu ya soka Tanzania Bara iliendelea jana kwa michezo miwili kuchezwa katika viwanja viwili tofauti.
Katika
uwanja wa Azam Complex Chamazi ,Azam fc imefanikiwa kupata points
zote tatu muhimu baaada ya kuifunga Afrikan Lyon kwa bao 1-0
lililofungwa na John Boko baada ya kupata pasi ya Kipre Tcheche
aliyeunasa mpira uliomtoka mlinda mlango wa Lyon.
Matokeo hayo yameifanya Azam kufikisha
jumla ya points 13 sawa na Simba ambao ndio mabingwa watetezi wa taji la
ligi hiyo na ambao kesho watakuwa wakishuka dimbani kucheza dhidi ya
JKT Oljoro ya Arusha mchezo ambao utachezwa katika uwanja wa Taifa
jijini Dar es Salaam.
Mchezo mwingine uliochezwa leo ni baina
ya Ruvu Shooting ya Pwani waliokuwa wenyeji wa Coastal Union ya Tanga
mchezo ambao umefanyika katika uwanja wa Mabatini Mlandizi.
Katika mchezo huo wenyeji JKT Ruvu
wamefanikiwa kuchomoza na ushindi wa mabao 2-0, matokeo ambayo
yamewafanya Ruvu kufikisha jumla ya points 9 na hivyo kukalia nafasi ya
tatu katika msimamo wa ligi hiyo.
0 comments:
Post a Comment