HASSAN Othman Hassan amechaguliwa tena kuwa mwenyekiti wa Chama cha Soka
Pwani (COREFA) huku nafasi ya katibu ikirudi tena kwa Riziki Majala.
Naye Geofrey Irick Nyange amechaguliwa kuwa Mjumbe wa Mkutano Mkuu TF,
Juma Haruna Kisoma Mwakilishi wa Klabu TFF na Abubakar Allawi
amechaguliwa kuwa Mhazini.
Waliochaguliwa kuwa Wajumbe wa Kamati ya Utendaji katika uchaguzi huo
uliofanyika kisiwani Mafia ni Musa Bakari Athumani, Godfrey Magnus Haule
na Gwamaka Oden Mlagila na mwakilishi wa Wanawake ni Florence
Ambonisye.
Akiongea na waandishi wa Habari Ofisa Habari wa Shirikisho la Soka
Nchini(TFF) Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) linatoa pongezi
kwa uongozi mpya wa Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Pwani (COREFA)
uliochaguliwa katika uchaguzi uliofanyika juzi.
Pia aliongeza kuwa ushindi waliopata viongozi waliochaguliwa kuongoza
chama hicho unaonesha jinsi wajumbe wa Mkutano Mkuu wa COREFA walivyo na
imani kubwa kwao katika kusimamia mchezo huo mkoani Pwani.
Pia alisema TFF inaahidi kuendeleza ushirikiano wake kwa Kamati ya
Utendaji ya COREFA chini ya uenyekiti wa Hassan Othman Hassan ambaye
amechaguliwa tena kuongoza chama hicho.
Wambura alisema uongozi huo mpya una changamoto nyingi, kubwa ikiwa ni
kuhakikisha unaendesha shughuli za mpira wa miguu mkoani Pwani kwa
kuzingatia katiba ya COREFA pamoja na vyombo vya mpira wa miguu vilivyo
juu yake.
"Pia tunatoa pongezi kwa Kamati ya Uchaguzi ya COREFA na Kamati ya
Uchaguzi ya TFF kwa kuhakikisha uchaguzi huo unaendeshwa kwa mujibu wa
kanuni za uchaguzi za wanachama wa TFF", alisema Wambura.
Monday, October 15, 2012
HASANOO NA KABURU WAULA PWANI
3:25 PM
No comments
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments:
Post a Comment