Michuano
ya Ligi Kuu ya Vodacom (VPL) kuwania ubingwan wa Tanzania Bara inaingia
raundi ya sita wikiendi hii kwa mechi saba. Kesho (Oktoba 6 mwaka huu)
African Lyon itakuwa mwenyeji wa Azam katika mechi itakayochezwa Uwanja
wa Azam Complex, Dar es Salaam kuanzia saa 10 kamili jioni.
Nayo
Ruvu Shooting itaikaribisha Coastal Union ya Tanga katika mechi
itakayochezeshwa na Oden Mbaga wa Dar es Salaam kwenye Uwanja wa
Mabatini ulioko Mlandizi mkoani Pwani. Mbaga atasaidiwa na Samuel
Mpenzu, Ferdinand Chacha na Andrew Shamba.
Jumapili
(Oktoba 7 mwaka huu) kutakuwa na mechi kati ya Simba na Oljoro JKT
itakayochezwa Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam, Kagera Sugar na Yanga
(Uwanja wa Kaitaba mjini Bukoba), Mgambo Shooting na Polisi Morogoro
(Uwanja wa Mkwakwani jijini Tanga), Toto Africans na JKT Ruvu (Uwanja wa
Kirumba jijini Mwanza) na Tanzania Prisons na Mtibwa Sugar (Uwanja wa
Kumbukumbu ya Sokoine jijini Mbeya).
Boniface Wambura
Ofisa Habari
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF)
0 comments:
Post a Comment