Press
Release
CHAMA CHA
MSALABA MWEKUNDU MKOA WA DAR ES SALAAM:
VOLUNTEERS NA WANACHAMA,
SLP 1133,
DAR ES
SALAAM.
WANACHAMA YAH: PINGAMIZI DHIDI YA MAJINA YA
BAADHI YA WAGOMBEA WA NAFASI ZA UONGOZI WA CHAMA CHA MSALABA MWEKUNDU MKOA WA DAR ES SALAAM WASIO NA VIGEZO.
Chama cha Msalaba Mwekundu mkoa wa Dar es Salaam: Volunteers na Wanachama, kwa
masikitiko makubwa, tunapenda kuelezea malalamiko yetu juu ya kukiukwa kwa taratibu za uchaguzi mkuu
wa chama Mkoa wa Dar es Salaam.
Kama wanachama, tunasikitika kuona baadhi ya
taratibu za msingi zinakiukwa kwa makusudi ili hali ni kinyume na taratibu
zinazoongoza chama chetu hasa taratibu zinazosimamia uchaguzi mkuu.
Jambo ambalo linatusikitisha zaidi ni namnba
ambavyo baadhi ya viongozi wetu wameshindwa kusaidia katika suala hili ambalo
kiukweli linaweza kurudisha nyuma hatarakati na maana halisi chama katika
kusaidia jamii inayotuzunguka.
Tatizo ambalo sisi wanachama tunalilalamikia ni
namna taratibu zilizoendesha mchakato wa zoezi zima la kuyakusanya na kuyachambua
majina ya wanachama walioomba nafasi mbali mbali za uongozi ngazi ya Mkoa wa
Dar Es Salaam na hatimaye siku chache zilizopita kuyatangaza
majina ya wagombea waliofuzu vigezo hivyo.
Uchaguzi huu wa mwaka 2012 ambao kimsingi
unakua wa kwanza kufanyika chini ya kanuni mpya za uchaguzi zilizopitishwa na
Bodi mwaka 2011.
Tofauti na miaka mingine, kanuni hizi zimejikita zaidi katika
kigezo cha elimu ya mgombea, mafunzo na ujuzi katika fani husika kwa mfano;
ngazi ya Matawi na Wilaya mgombea lazima
awe na elimu ya kidato cha nne, Mkoani lazima awe na elimu isiyopungua kidato
cha sita na Taifa awe na shahada ya kwanza.
Pamoja na
kanuni hizo za wazi, lakini badi zimeshindikana kufanyika, tunadhani kanuni
hizo hazikuzingatia kanuni kuu saba za msalaba mwekundu.
Baadhi ya wagombea
waliopitishwa kugombea nafasi hizo tunaamini wazi kuwa hawakustahili kwa
kuzingatia kigezo cha elimu kwamba hawakufikia elimu iliyokuwa inahistajika kwa
ngazi ya mkoa, (yaani hawana elimu ya kidato cha sita) na kuwaacha wale wenye
sifa hizo na nyinginezo.
Majina hayo ni Amina
Mwalimu (Mafunzo na Uuguzi), Hidan
Ricco (Makamu Mwenyekiti), Subira Tamla
(Mafunzo na Uuguzi), Edson Kanisa (Maafa na Habari) Mayasa Bashele (Jinsia) Francis Msisi (Maafa
na Habari).
Kutokana na makosa hayo ndiyo maana tunaona
kuna sababu ya uchaguzi huo kusimamishwa
badala ya kufanyika Oktoba 27 mwaka 2012 ili kutoa nafasio kwa mchakato
huo kufanyika kwa upya kwa ajili yan kuitendea
hali taasisi kutokana na heshima kubwa iliyonayo mbele ya jamii.
pia tunaambatanisha na barua ambayo
tulimwandikia Mwenyekiti wa Taifa ya Oktoba 16 2012 na nakala kumpatia Katibu
Mkuu Chama Cha Msalaba Mwekundu Taifa.
0 comments:
Post a Comment