TIMU ya Simba ya Dar es salaam leo imewazamisha wanajeshi wa JKT Oljoro kwa bao 4-1, mchezo uliochezwa uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam
Simba ilijipatia bao la kwanza kupitia kwa Amri Kiemba dk 16 aliyeachia shuti kali lililomshinda mlinda mlango wa JKT Oljoro.
Baada ya bao hili JKT waliliandama lango la Simba na kujipatia bao la kusawazisha kupitia kwa Paulo Nonga dk 29 kwani mabeki wa Simba walikuwa wametoka hivyo ikawa rahisi kwa Nonga kumpiga chenga Juma Kaseja aliyekuja kuucheza.
Kabla ya kwenda mapumziko Kiemba tena aliwanyanyua mashabiki kwa kufunga bao lilingine baada ya mpira wa krosi uliopigwa na Nassoro Masoud.
Timu zilikwenda mapumziko matokeo yakiwa 2-1
Baada ya kurudi mapumziko timu zote zilishambuliana kwa zamu lakini dk 83 Emanuel Okwi akifungia Simba bao la tatu baada ya kupokea krosi safi toka kwa Nassoro Masoud "Cholo"
Kwenye muda wa nyongeza Simba ilijipatia bao la penalti lililofungwa na Felex Sunzu baada ya mlinda mlango wa JKT Oljoro kumfanyia faulo mbaya wakati akienda kufunga bao na mwamuzi kumwonyesha kadi nyekundu.
Mpaka dk tisini zinamalizika matokeo ni kuwa Simba wameshinda kwa bao 4-1 hata hivyo JKT itajutia mchezo huu kwani wachezaji wake wawili walionyeshwa kadi nyekundu kutokana na kucheza mchezo ambao siyo wa kiungwana.
Kocha wa JKT Mbwana Makata amesema timu yake imefungwa na mabao yaliyofugwa hana shaka nayo kwani timu imecheza chini ya kiwango na ni mchezo wa kwanza timu yake kupoteza.
0 comments:
Post a Comment