Tuesday, October 9, 2012

YANGA YACHAPWA NA KAGERA SUGAR KAITABA

Kikosi cha Yanga

Yanga ya jijini Dar es salaam kwa mara nyingine imezidi kupoteza matumaini ya kutwaa ubingwa wa ligi kuu soka Tanzania Bara msimu huu baada ya kukubali kipigo cha goli 1-0 na Kagera Sugar ya mkoani Kagera.
Hadi dakika 45 za kipindi cha kwanza zilipo kamilika timu zote mbili zilikuwa  hazija fungana kipindi cha pili kilianza kwa kasi huku kila timu ikitafuta goli  la kuongoza, goli pekee la Kagera lililopeleka kilio katika makutano ya mitaa ya twiga na jangwani limefungwa kunako dakika ya 67 na mshambuliaji  Themi Felix Buhaja. 
Matokeo hayo yanazidi kuiweka Yanga katika mazingira magumu na imeporomoka katika msimamo wa ligi kuu ya Tanzania Bara hadi nafasi ya Saba kutokanana michezo sita iliyokwisha cheza imeshinda michezo miwili imefungwa michezo miwili na imetoka sare michezo miwili na imejikusanyia pointi nane tu,tofauti na watani wao wa jadi Simba inayoongoza ligi kuu soka Tanzania Bara ikiwa imejikusanyia point 16 ikiwa imeshuka dimbani mara sita sawa na Yanga imeshinda michezo 5 na imetoka sare mchezo mmoja na hadi sasa ndiyo timu pekee ambayo haijapoteza mchezo wowote


0 comments: