Monday, September 17, 2012

MIRAMBO VETERAN ZATOKA SARE NA MUHIMBILI 2-2

Mchezaji wa Mirambo akiwa na mpira huko mchezaji wa Muhimbili akimkimbiza kwwenye mchezo wa kirafiki uliochezwa jana uwanja wa Muhimbili na kutoka sare 2-2


Mchezaji wa Muhimbili aliyevaa jezi nyekundu akijaribu kumtoka mchezaji wa Mirambo jana kwenye mchezo wa kirafiki uliochezwa uwanja wa Muhimbili


TIMU za Veteran za Muhimbili na Mirambo zimetoshana nguvu kwa kutoka sare ya kufungana bao 2-2 kwenye mchezo uliochezwa juzi jioni kwenye uwanja wa Muhimbili.

Mchezo huo ulikuwa wa kuvutia sana kwani wachezaji hao wa zamami waliocheza ligi kuu walionyesha mbwembwe zao kwa pasi za kuonana na si kukimbia na mpira kama mtu anayefukuzwa.

Mpaka kipindi cha kwanza kinamalizika hakuna timu iliyokuwa imeliona lango la mpinzani kutokana na umahiri wa beki kuwa makini.

Kipindi cha pili kilianza kwa kila timu kufanya mabadiliko na Muhimbili ndio waliokuwa wa kwanza kuliona lango la mashujaa wa Tabora Mirambo waishio hapa Dar es salaam kupitia kwa Clement Kahabuka.

Baada ya kufungwa bao hilo Mirambo walizinduka na ndipo Idd Moshi akasawazisha bao kwa shuti kali lilomshinda mlinda mlango wa Muhimbili.

Bao lingine la Mirambo lilifungwa na Wakulichombe Salum kwa shuti baada ya kutokea piga nikupige langoni mwa Muhimbili. Beki ya Mirambo ilijitahidi kulinda goli lakini ilijikuta Muhimbili wakisawazisha bao kupitia kwa Akida Makunda na kufanya matokeo yawe 2-2 hadi mwisho wa mchezo.

Wachezaji wa Mirambo walijikuta wanamlalamikia mwamuzi wakidai bao alilofunga Makunda mpira ulikuwa umetoka nje na kufanya mchezo kusimama takribani dk 3 kabla ya kuendelea tena.

0 comments: