Friday, June 15, 2012

Simba yalegezea bilioni 2 za Okwi



Ezekiel Kamwaga  msemaji wa Simba

Na Mwandishi Wetu
KLABU ya Simba imelegeza msimamo wake baada ya kusema kuwa dau la sh bilioni mbili iliyokuwa imetangaza awali kwa klabu inayotaka kumsajili mshambualiaji wake, Emmanuel Okwi kuwa linaweza kupungua au kuongezekana.
Akizungumza na tanzaniacelebrity.com msemaji wa Simba, Ezekiel Kamwaga alisema kuwa Simba itakuwa tayari kufanya mazungumzo juu ya dau halisi la nyota huyo ambapo dau hilo litategemea klabu inayomuita inaweza kutoa kiasi gani cha fedha.
Kwa sasa Okwi ameitwa katika majaribo nchini Afrika Kusini katika klabu ya Orlando Pirates ambapo kama akifuzu ndiyo mazungumzo ya uhamisho wake yatafanyika.
 “Tupo tayari kumwachia kwa dau tutakalokubaliana lakini kwa hivi sasa tunachoangalia ni kumsaidia kwa hali na mali ili aweze kwenda na kufuzu majaribio yake kwani itakuwa ni sehemu muhimu ya kuitangaza klabu yetu.
 “Ni kweli awali tulitangaza dau hilo lakini kwa sasa tunasubiri kwanza kama atafuzu ndiyo tutakuwa kwenye wakatiu mzuri wa kujua anasajiliwa kwa kikasi gani kwa sababu  itategemea klabu inaweza kutoa kiasi gani.
 “Kimsingi kama unavyojua katika usajili huwa kunakuwa na mambo mengi lakini imani nyetu ni kwamba Simba inaweza kumuachia Okwi kwa dau lolote kwa kuwa linaweza kuongezeka au kupungua,” alisema Kamwaga.
Awali Simba ilitangaza kumuachia Okwi kwa dau la sh bilioni mbili kwa klabu ambayo ilikuwa inahitaji kumsajili nyota huyo ambaye ameonyesha kiwango cha juu katika msimu wa uliopita.
Tayari klabu ya Orlando ya Afrika Kusini imeonekana kumhitaji mshambuliaji huyo mwepesi kwenye kikosi chake kwa ajili ya Ligi Kuu ya Afrika Kusini.
Kabla ya kutua Simba, Okwi alikuwa akiitumikia klabu ya SC Villa tangu mwaka 2009 ambapo alifanikiwa kuifungia timu hiyo mabao 13 katika mechi 40 alizocheza. Hadi sasa ameipa Simba mabao 17 kati ya  mechi 27 alizocheza tangu mwaka 2010 alipojiunga na mabingwa hao wa Ligi ya Tanzania Bara.

0 comments: