Monday, June 18, 2012

nyota Yanga atua Coasta

 
Aliyekuwa shambuliaji nyota wa kikosi cha Yanga B, Atupele Green amejiunga na klabu ya Coastal Union kwa mkataba wa miaka mitatu ikiwa  ni maandalizi ya Ligi Kuu Tanzania Bara.

Akizungumza na Smtandao huu, Green alisema kuwa amevutiwa na dau alilopewa na Coastal ambapo ameongeza kuwa anaimani kuwa atapata nafasi ya kucheza zaidi tofauti na klabu nyingine.

Kadhalika amefafanua kwmaba hana mpango na kucheza katika klabu za Simba wala Yanga kwani anachikiangalia kwa sasa ni kucheza soka la kulipwa.

“Nimeona kwamba hapa ndipo patakapokuw ana maisha bora ya baadaye kwenye soka langu, imani yangu ni kwmaba nitaweza kupata mafanikio makubwa katika siku zijazo hivyo sina shaka.

“Nihitaji kucheza soka kwa muda mrefu zaidi ambapo ili kufanya hivi ni lazimia kwenye  klabu ninatakayopata nafasi ya kutumika.

“Ninachikiamini ni kwamba, nataka kufanya kazi kubwa kwa ajili ya nchi hii ninaangalia namna bora ya kuweza kutangaza jina langu na nchi yangu hivyo hapa Coastal ndiyo nimeona panaweza kunifaa ndiyo maana nimekubali kuja.

“Pia nimepewa dau nililokuwa nalihitaji kwa kama nilivyokuwa nimepanga akilini mwangu,” alisema Green ambaye aliitumikia Yanga miaka mitano.

Katika hatua nyingine nyota huyo amesisitiza  kuwa baada ya mkataba wake kumalika ataangalia kucheza soka la kulipwa nje ya nchi na hatakuwa na mpango wa kucheza kwenye Ligi kuu ya Tanzania Bara.

Awali Green alikuwa asajiliwe na Yanga lakini ilitokea hali ya kutoelewana baina ya pande hizo mbili hali iliyofanya mkataba uliyokuwa umeandaliwa kwa ajili yake kuchanwa hadharani.

0 comments: