Monday, October 15, 2012

13 WAPITISHWA KUGOMBEA TWFA

WAGOMBEA 13 kati ya 15 waliojitokeza kuwania nafasi mbalimbali za uongozi kwenye Chama cha Soka la Wanawake Tanzania (TWFA) wamepitishwa baada ya usaili uliofanyika juzi.

Kwa mujibu wa Mwenyekiti wa Kamati ya Uchaguzi ya TWFA, Ombeni Zavala, waliopitishwa kwenye nafasi ya  Mwenyekiti ni Isabellah Husein Kapera, Joan Ndaambuyo Minja na Lina Paul Kessy.

Makamu Mwenyekiti ni Rose Kisiwa wakati wanaowania nafasi ya Katibu Mkuu ni Amina Ali Karuma na Cecilia Oreste Makafu.

Mgombea pekee wa nafasi ya Katibu Msaidizi, Macky Righton Mhango naye amepita kwenye usaili huo na kwenye nafasi ya Mhazini ni Rose Stewart Msamila.

Furaha Francis na Zena Chande wamepitishwa kuwania nafasi ya Mjumbe wa Mkutano Mkuu wa Shirikisho la Soka nchini (TFF) wakati waliopita kuwania ujumbe wa Kamati ya Utendaji ya TWFA ni Triphonia Ludovick Temba, Rahim Salum Maguza na Sophia James Charles.


Wagombea wawili ambao hawakupitishwa kwa ajili ya uchaguzi huo
unaotarajiwa kufanyika Novemba 4 mwaka huu ni Julliet Mndeme na Jasmin Soud walioomba ujumbe wa Mkutano Mkuu wa TFF kwa sababu hawakufika kwenye usaili pia walikuwa wamewekewa pingamizi.

0 comments: