Friday, October 26, 2012

Press Release




Press Release
CHAMA CHA MSALABA MWEKUNDU MKOA WA  DAR ES SALAAM: VOLUNTEERS NA WANACHAMA,
SLP 1133,
DAR ES SALAAM.






WANACHAMA YAH: PINGAMIZI DHIDI YA MAJINA YA BAADHI YA WAGOMBEA WA NAFASI ZA UONGOZI WA CHAMA  CHA MSALABA MWEKUNDU MKOA WA   DAR ES SALAAM WASIO NA VIGEZO.


Chama cha Msalaba Mwekundu mkoa wa  Dar es Salaam: Volunteers na Wanachama, kwa masikitiko makubwa, tunapenda kuelezea malalamiko yetu  juu ya kukiukwa kwa taratibu za uchaguzi mkuu wa chama Mkoa wa Dar es Salaam.

Kama wanachama, tunasikitika kuona baadhi ya taratibu za msingi zinakiukwa kwa makusudi ili hali ni kinyume na taratibu zinazoongoza chama chetu hasa taratibu zinazosimamia uchaguzi mkuu.

Jambo ambalo linatusikitisha zaidi ni namnba ambavyo baadhi ya viongozi wetu wameshindwa kusaidia katika suala hili ambalo kiukweli linaweza kurudisha nyuma hatarakati na maana halisi chama katika kusaidia jamii inayotuzunguka.

Tatizo ambalo sisi wanachama tunalilalamikia ni namna taratibu zilizoendesha mchakato wa zoezi zima la kuyakusanya na kuyachambua majina ya wanachama walioomba nafasi mbali mbali za uongozi ngazi ya Mkoa wa Dar Es Salaam na hatimaye siku chache zilizopita  kuyatangaza  majina ya wagombea waliofuzu vigezo hivyo.

Uchaguzi huu wa mwaka 2012 ambao kimsingi unakua wa kwanza kufanyika chini ya kanuni mpya za uchaguzi zilizopitishwa na Bodi mwaka 2011.

Tofauti na miaka mingine, kanuni hizi zimejikita zaidi katika kigezo cha elimu ya mgombea, mafunzo na ujuzi katika fani husika kwa mfano; ngazi ya Matawi na Wilaya  mgombea lazima awe na elimu ya kidato cha nne, Mkoani lazima awe na elimu isiyopungua kidato cha sita na Taifa awe na shahada ya kwanza.


Pamoja na kanuni hizo za wazi, lakini badi zimeshindikana kufanyika, tunadhani kanuni hizo hazikuzingatia kanuni kuu saba za msalaba mwekundu. 

Baadhi ya wagombea waliopitishwa kugombea nafasi hizo tunaamini wazi kuwa hawakustahili kwa kuzingatia kigezo cha elimu kwamba hawakufikia elimu iliyokuwa inahistajika kwa ngazi ya mkoa,  (yaani hawana elimu ya kidato cha sita) na kuwaacha wale wenye sifa hizo na nyinginezo.

Majina hayo ni  Amina Mwalimu  (Mafunzo na Uuguzi), Hidan Ricco  (Makamu Mwenyekiti), Subira Tamla (Mafunzo na Uuguzi), Edson Kanisa (Maafa na Habari)  Mayasa Bashele (Jinsia) Francis Msisi (Maafa na Habari).

Kutokana na makosa hayo ndiyo maana tunaona kuna sababu ya uchaguzi huo kusimamishwa  badala ya kufanyika Oktoba 27 mwaka 2012 ili kutoa nafasio kwa mchakato huo  kufanyika kwa upya kwa ajili yan kuitendea hali taasisi kutokana na heshima kubwa iliyonayo mbele ya jamii. 

pia tunaambatanisha na barua ambayo tulimwandikia Mwenyekiti wa Taifa  ya Oktoba 16 2012 na nakala kumpatia Katibu Mkuu Chama Cha Msalaba Mwekundu Taifa.

0 comments: