Monday, July 2, 2012

MANJI AZUA 'BALAA' TFF, UCHAGUZI YANGA WAINGIA KIZA

Manji anaondoka TFF, umati ukimsindikiza

Sura za huzuni; wanachama wakisikitika nje ya ofisi za TFF

Wanachama wakisikitikia pingamizi la Manji

Ni huzuni tupu

Hakuna anayufurahia 

Kila mtu ana hasira

Yaani watu wamekasirika ile mbaya

Hadi akina mama wana hasira pia

Manji anatoka chumba cha mahojiano

Anaziacha ofisi za TFF

Anapotea

Anawasalimu wazee

Anajadiliana na wazee

Umati unamsindikiza

Anafunguliwa mlango wa gari lake

Anaingia na kupotea

Na Prince Akbar
MAMIA ya wanachama wa klabu ya Yanga ya Dar es Salaam, leo wameandamana hadi makao makuu ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Ilala, Jijini kupinga pingamizi alilowekewa mgombea Uenyekiti wa klabu hiyo katika uchaguzi wa Julai 15, mwaka huu, Yussuf Manji.
Kamati ya Uchaguzi ya TFF, chini ya Mwenyekiti wake, Deo Lyatto leo ilikuwa inapitia pingamizi mbili walizowekewa wagombea, Manji na Stanley Kavela ‘Yono’ anayewania Umakamu Mwenyekiti.
Tangu saa nne asubuhi hadi saa nane mchana, Kamati hiyo ilikuwa inamuhoji Manji ambaye hata alipotoka, ilielezwa alitakiwa kurejea tena.
Manji alitoka mara mbili na kurejea kufuata vielelezo alivyotakiwa kuwasilisha kuhusiana na pingamizi alilowekewa, ambalo vyanzo vinasema ni zito.
Tangu asubuhi wanachama walikuwa ‘kibao’ nje ya Ofisi za TFF, zilizopo ndani ya Uwanja wa Karume, Ilala, Dar es Salaam wakionyesha hasira zao dhidi ya pingamizi hilo, ambalo aliloliweka anafanywa siri.
Wanachama walisikika wakisema kwamba kama Kamati ya Lyatto itamuengua Manji basi hakuna haja ya uchaguzi.
Miongoni mwa waliokuwapo katika wanachama ni wazee wa klabu hiyo, akina Ibrahim Akilimali, Dk Idrisa Katundu na wengineo, wakiwemo wanachama maarufu.
Kuna kila dalili kwamba uamuzi wa kumuengua Manji katika uchaguzi huo litakuwa jambo la hatari kwa klabu hiyo, kwani wanachama tayari wamekwishajenga imani kubwa juu yake.   
Manji mwenyewe alipotoka kwenye chumba cha mahojiano alionekana asiye na furaha hali ambayo ilizidi kuwatia wasiwasi wanachama kwamba huenda kikao hakikuwa kizuri kwake.
 
PICHA NA HABARI KWA ZINATOKA MTANDAO WA BIN ZUBERY

0 comments: