Na Mahmoud Zubeiry
KAMATI ya
Ligi ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) ilikutana jana (Septemba 25 mwaka
huu) kupitia ripoti za mechi 21 za Ligi Kuu ya Vodacom ambazo zimeshachezwa
mpaka sasa, na kumuondoa George Komba aliyekuwa Kamisaa kwenye mechi namba 20
kati ya Simba na Ruvu Shooting, upungufu uliojitokeza katika ripoti yake.
Ofisa Habari
wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Boniphace Wambura Mgoyo ameiambia BIN
ZUBEIRY mchana huu kwamba, klabu ambazo zimeandikwa barua za onyo ni
African Lyon kwa kwenda uwanjani na jezi tofauti na zile ilizoonesha kwenye
mkutano wa maandalizi ya mechi (pre match meeting), Mtibwa Sugar kwa kuchelewa
kuwasilisha leseni za wachezaji wake wakati wa mechi na Ruvu Shooting kwa
ushangiliaji uliopita kiasi kwenye mechi yao dhidi ya Simba.
Amesema Kamati
pia imethibitisha kadi nyekundu ya Emmanuel Okwi kwa kumpiga kiwiko Kessy
Mapande wa JKT Ruvu, hivyo kwa mujibu wa Kanuni ya 25(1) anakosa mechi tatu na
kulipa faini ya sh. 500,000. Mchezaji huyo atakosa mechi namba 20, 27 na 80.
Amesema kwa
upande wa waamuzi, Ronald Swai ameandikiwa barua ya onyo kutokana na upungufu
alioonesha kwenye mechi kati ya Simba na Ruvu Shooting iliyochezwa Uwanja wa
Taifa, Dar es Salaam.
Amesema wamiliki
wa viwanja vya Mkwakwani, Tanga na Kumbukumbu ya Sokoine, Mbeya wameandikiwa
barua ya kuvifanyia marekebisho viwanja vyao katika maeneo mbalimbali yenye
upungufu ikiwemo uzio wa kutenganisha wachezaji na washabiki.
Aidha, Wambura
amesema beki Faustine Lukoo wa Polisi Moro ambaye kwa mujibu wa ripoti ya
mwamuzi aliyemtoa nje kwa kadi nyekundu alimtukana mchezaji mwenzake kwenye
mechi dhidi ya African Lyon na Katibu wa Oljoro JKT aliyemwaga maji kwenye
chumba cha timu ya Polisi Moro, masuala yao ni ya kinidhamu, hivyo yamepelekwa
Kamati ya Nidhamu na Usuluhishi kwa ajili ya hatua zaidi.
Amesema klabu
ambazo timu zao mpaka sasa zinacheza mechi bila kuwa na logo ya mdhamini, suala
hilo limepelekwa kwa wadhamini Vodacom kwa vile wenyewe ndiyo wanaogawa vifaa
hivyo.
Wakati huo
huo: Rais wa TFF, Leodegar Tenga atakutana na waandishi wa habari kesho mchana,
kwenye ukumbi wa mikutano wa TFF.
Katika hatua
nyingine, Kamati ya Uchaguzi ya TFF iliyokutana jana kusikiliza rufaa ya Mussa
H. Mahundi, Abou O. Sillia na Alex Mgongolwa dhidi ya Kamati ya Uchaguzi ya
Chama cha Soka Iringa (IRFA), iliyoomba Kamati ya Uchaguzi ya TFF kubatilisha
matokeo ya uchaguzi wa IRFA uliofanyika Septemba 8 mwaka huu Mufindi, Iringa,
na kuomba uchaguzi huo ufanyike upya kwa kuendeshwa na kusimamiwa na Kamati ya
Uchaguzi ya TFF, imetupilia mbali rufaa hiyo.
Kwa mujibu
wa Mwenyekiti wa Kamati ya Uchaguzi ya TFF, Deogratias Lyatto, baada ya kupitia
maelezo ya warufani na warufaniwa, Kamati ya Uchaguzi ya TFF imejiridhisha kuwa
rufani iliyowasilishwa mbele yake na Mahundi, Sillia na Mgongolwa ilikosa sifa
ya kuwa rufani kwa mujibu wa Kanuni za Uchaguzi za Wanachama wa TFF, Ibara ya
8(2), Ibara ya 21(3) na 24(2). Kwa kutozingatia matakwa ya Kanuni za Uchaguzi
za Wanachama wa TFF, Kamati ya Uchaguzi ya TFF imetupa rufani hiyo.
Kamati ya
Uchaguzi ya TFF imeiagiza Kamati ya Uchaguzi ya IRFA kuchukua hatua dhidi ya
Abuu Changawa kama ilivyoainishwa kwenye Kanuni za Uchaguzi za Wanachama wa
TFF, Ibara ya 28(6) kwa kuingilia mchakato wa uchaguzi wa IRFA siku ya
uchaguzi.
HIVI NDIVYO AGNES YAMO ALIVYOAGWA LEO, NI VILIO HADI KUZIRAI
Mwili wa
aliyekuwa Mwandishi wa Habari wa gazeti la Tanzania Daima, Agness Christopher Yamo
umeagwa leo mchana Buguruni, Dar es Salaam, tayari kwa safari ya mazishi kesho
mjini Morogoro. Yamo aliyewahi pia kufanya New Habari 2006 Limited, alifariki
dunia jana katika hospitali ya Jeshi, Lugalo, Dar es Salaam, alikokuwa amelazwa
kwa matibabu.
Katika uagwaji
wa mwili wa marehemu, aliyekuwa mcheshi na rafiki wa wengi, mamia walijitokeza
na wengi walishindwa kujizuia kiasi cha kulia hadi kupoteza fahamu. Hakika ilikuwa
huzuni, simanzi na majonzi eneo la tukio. Agness ameliza watu. Mungu aiweke
pema peponi roho ya marehemu, Amin.
Waombolezaji |
Waombolezaji |
Mhariri Mtendaji wa Tanzania Daima, Absalom Kibanda |
Mkurugenzi wa Tanzania Daima, Lillian Mbowe |
+255 757 444455 or princezub@hotmail.com
Mahmoud Zubeiry
at
5:41:00 AM
No comments:
Links to this post
Links to this post
Reactions: |
Subscribe to:
Posts (Atom)