Sunday, September 30, 2012

SIMBA NOMA YAUA IKIWA PUNGUFU

Wachezaji wa Simba wakishangilia bao alilofunga Sunzu kwenye mchezo uliochezwa jana uwanja wa Taifa na Simba kushinda bao 2-1

Mshambuliaji wa Simba Felex Sunzu akiwatoka mabeki wa Prison kwenye mchezo uliochezwa uwanja wa Taifa jana jioni

Baadhi ya Mashabiki wa Simba waliokuwepo uwanjani
TIMU ya Simba jana iliifunga Prison ya Mbeya bao 2-1 ikiwa pungufu baada ya beki wao Amir Maftah kuonyeshwa kadi nyekundu.

Prison ndio walikuwa wa kwanza kuliona lango la Simba dakika ya sita baada ya shuti la Lugano Mwangama kubabatiza beki wa Simba na kupoteza uelekeo hivyo kumchanganya Juma Kaseja na kutinga wavuni

Dk 44 Felex Sunzu alisawazisha bao hilo kabla ya Mrisho Ngassa kuhitimisha karamu ya mabao kuwa 2-1

0 comments: