Sunday, September 23, 2012

KOCHA YANGA ATIMULIWA

Kocha Tom Saintfiet akiwa kwenye benchi la ufundi la Yanga kabla hajatimuliwa
KOCHA wa Yanga Tom Saintfiet amefukuzwa baada ya kutofautiana na uongozi wa Yanga na Yanga sasa itakuwa chini ya kocha msaidizi Fredy Felex Minziro

Mbeligiji huyo amefukuzwa baada ya kikao kilichokaa makao makuu ya klabu, makutano ya mitaa ya Twiga na Jangwani.

Mapema jana asubuhi akitangaza maamuzi ya kamati kuu Makamu Mwenyekiti wa Yanga, Clement Sanga alisema kuwa kocha huyo wamesitisha mkataba naye kutokana na kutoheshimu maamuzi na mipaka ya kazi yake.

Jana asubuhi kamati hiyo iliwafukuza kazi Sekretarieti nzima ya klabu, akiwemo Katibu Celestine Mwesigwa na Ofisa Habari, Louis Sendeu, kutokana utendaji usioridhisha.

Wengine ni Masoud Saad, aliyekuwa Ofisa Utawala, Philip Chifuka aliyekuwa Mhasibu na Hafidh Saleh aliyekuwa Meneja ambaye anahamishiwa kwenye majukumu mengine.

Kwa ujumla maamuzi haya yanakuja baada ya Yanga kuanza vibaya Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara, ikiambulia pointi moja tu katika mechi zake mbili za awali, kutokana na sare ya bila kufungana na Prisons kwenye Uwanja wa Sokoine mjini Mbeya Jumamosi na Jumatano ikachapwa mabao 3-0 Morogoro Uwanja wa Jamhuri, Morogoro.

Lawrence Mwalusako ameteuliwa kukaimu nafasi ya Katibu wa klabu hiyo na Mkurugenzi wa fedha na mipango Denis Owindo.

0 comments: