TIMU ya Yanga ya Dar es salaam leo imezinduka usingizi na kuipatia
kichapo JKT Ruvu bao 4-1 kwenye uwanja wa taifa mbele ya Yusuf Manji.
Yanga ambayo ilicheza kwa kujiamini sana na kushambulia muda wote
ilijipatia mabao yake kupitia kwa Nadir Haroub Canavaro, Didier
Kavumbagu ambaye alifunga mawili na Mshambuliaji Kinda Simon Msuva
alihitimisha idadi ya mabao.
Michezo mingine iliyochezwa ni Azam 1 vs Mtibwa 0 ulichezwa Chamazi
JKT Oljoro 1 vs Polisi Moro ulichezwa Sheikh Aman Karume Arusha
Toto African 1 vs Coastal Union ulichezwa Mkwakwani Tanga.
Leo kutakuwepo na michezo ya
Simba vs Ruvu Shooting utakaochezwa Uwanja wa Taifa
Mgambo JKT vs Kagera Sugar uwanja wa Mkwakwani Tanga
African Lyon vs Tanzzania Prison uwanja wa Chamazi
|
Beki Sostenes Manyasi wa JKT Ruvu akimdhibiti mshambuliaji wa Yanga Hamis Kiiza kwenye mchezo uliochezwa uwanja wa Taifa jana, Yanga ilishinda 4-1 |
|
Benchi la Ufundi likiongozwa na Felex Minziro ambaye anashikilia mokoba ya kocha Tom Saintfiet aliyetupiwa virago jana. |
|
Wachezaji wa Yanga wakishangilia bao alilofunga Nadir Haroub Canavarokwenye mchezo wo na JKT Ruvu uwanja wa Taifa jana |
0 comments:
Post a Comment