Saturday, September 29, 2012

AZAM YAIENGUA SIMBA KILELENI

Golikipa wa JKT RuvuShaban Dihile akidaka mpira uliokuwa unaelekea golini mwao huku beki Hussein  Dumba akimzuia John Bocco asilete madhara
Mchezo wa ligi kuu ya soka Tanzania Bara kati ya Azam na JKT Ruvu uliofanyika katika uwanja wa taifa jijini Dar es Salaam umemalizika kwa Azam kupata ushindi wa mabao 3-0 ambapo mabao ya washindi yakiwekwa nyanvuni na John Bocco akifunga bao la kwanza kwa njia ya mkwaju wa penati na mabao mengine mawili yakiwekwa nyavuni na mshambiliaji Pipre Tcheche.
Kwa matokeo hayo Azam imefikisha jumla ya points 10 na kukalia usukani wa ligi hiyo ikifuatiwa na bingwa mtetezi Simba wenye points 9 na Coastal ikiwa katika nafasi ya tatu baada ya kukusanya jumla ya points 7.
Changamoto kubwa iliyojitokeza ni licha ya mchezo huo uliochezwa usiku na kupata nafasi ya kuonyeshwa moja kwa moja na kituo cha television cha Supersport, lakini mpira mbovu na mashabiki wachache wamefanya mchezo huo  kuonekana kutostahili kupata nafasi onyesho moja kwa moja kwani uwanja ulionekana kwenye kichupa ukiwa mweupe kiasi mpiga picha kupata wakati mgumu kuchukua sehemu ya watazamaji.
Hata hivyo lawama kwa mara nyingine zimeelekezwa kwa shirikisho la soka nchini kwa kuweka kiingilio cha juu cha shilingi 5,000 na 10,000 katika mchezo ambao timu zake hazina mashabiki wengi kama ilivyo vilabu vya Simba na Yanga.
Ligi hiyo inaendelea tena leo tarehe 29/09/2012 ambapo Simba itakuwa mwenyeji wa maafande wa Tanzania Prisons uwanja wa Taifa mchezo ambao utaanza saa 11jioni na kesho  tarehe 30/09/2012 Yanga ataikaribisha Coastal Union ya Tanga katika uwanja huo huo na kuonyeshwa live kama ilivyokuwa mechi ya leo.

0 comments: