Sunday, September 16, 2012

SIMBA YAANZA VEMA KUTETEA UBINGWA

Mshambuliaji wa kimataifa wa Simba Daniel Akuffo akijaribu kumtoka mchezaji wa African Lyon wakati wa mechi ya ufunguzi wa pazia la ligi kuu bara.
TIMU ya Simba ya Dar es salaam imeanza vizuri kulitetea kombe lake la ligi baada ya kuifunga African Lyon bao 3-0 mchezo uliochezwa uwanja wa taifa jijini Dar es salaam.
Mabao ya Simba yalifungwa na Emanuel Okwi, Cholo na  Daniel Akuffo ambaye alifunga kwa penati baada ya Okwi kufanyiwa fauli eneo la penati
Simba waliutawala mchezo sana hivyo matokeo waliyopata ya 3-0 walistahili sana.

Matokeo mengine ni kama ifuatavyo
Uwanja wa Sokoine Mbeya Yanga 0-0 na Prison
Uwanja wa Kaitaba Kagera Azam 1-0 Kagera Sugar bao lilifungwa na Humudu

Uwanja wa Jamhuri Morogoro Mtibwa  Sugar 0-0 Polisi Moro
Uwanja wa Chamazi Dar JKT Ruvu 2-1 Ruvu Shooting
Uwanja wa Mkwakwani Tanga Coastal Union 1-0 JKT Mgambo
Uwanja wa CCM Kirumba Toto African   1-1     JKT Oljoro

0 comments: